Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack ametoa agizo hilo akiongoza kikao cha Kamati ya Lishe ya Mkoa kilichofanyika tarehe 09 Machi 2024 katika ukumbi wa Ofisi yake.
Mhe. Telack amewataka Maafisa Kilimo kutoa elimu ya kilimo bora kwa kuzingatia utaalam ili wakulima wazalishe kwa tija na mavuno ya kutosha.
Amesema kuwa elimu hiyo itolewe kwa wakulima pamoja na shule ambazo zinalima huku akisisitiza kuwa kwa kipindi hiki cha mwezi Machi mvua zimepungua hivyo waelekezwe aina ya mazao yanayoweza kuzalishwa Kwa kipindi cha mvua kilichobaki.
Elimu ya kilimo bora itasaidia uzalishaji mzuri wa chakula mashuleni jambo ambalo litaimarisha upatikanaji wa chakula kwa wanafunzi hivyo kuongeza uelewa na kupunguza utoro.
Amesisitiza kuwa kilimo bora kitasaidia kupunguza na kuondoa changamoto ya uhaba wa chakula na hivyo kuimarisha lishe kwa watoto, mama wajawazito na jamii kwa ujumla.
Mwisho, Mhe. Telack amewataka Maafisa elimu na Wakuu wa Shule kusimamia na kutoa taarifa za shule zote zinazozalisha chakula kupitia mashamba yalioyopo mashuleni.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.