Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack ameyasema hayo jana katika kikao cha kujadili mwongozo na utekelezaji wa ugawaji wa pembejeo za korosho kwa msimu wa 2022/2023 ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Telack amekemea tabia ya viongozi wa vyama vya ushirika kuwadhurumu wakulima fedha za mazao yao na kusababisha malalamiko. Amewataka viongozi wa vyama hivyo kusimamia vizuri mfumo mzima wa uuzaji wa zao la ufuta ikiwemo kutumia vizuri mizani na kusimamia vizuri malipo ya wakulima ili mkulima apate haki yake kulingana na alichozalisha, huku akisisitiza ushirika sio duka la wizi.
“Usimamizi wa upimaji wa ufuta wakulima watakaoleta, kuna kuangalia mizani lakini kuangalia ubora, msiwapunje wakulima, ninaomba sana msiwapunje wakulima, na niagize wenzetu wa vipimowapite kuhakiki mizani zote sasa ili wakulima wetu waweze kupata haki……..”
“Lakini niwaombe pia viongozi wa amcos, viongozi wa vyama vikuu vya ushirika wakasimamie malipo ya wakulima……..malipo yatoke vile vile kwa wakati ili kuepusha malalamiko kwa wananchi.”
“Niwaombe viongozi mnaopewa dhamana kwenye vyama vya ushirika, huko sio duka la wizi, kwenye ushirika sio kwenye kichaka cha wizi…………..tumuogope mungu.”
Mhe. Telack ameendelea kusisitiza kuwa vyama vya msingi vitakavyoshindwa kuwalipa wakulima vitakosa sifa ya kununua korosho au ufuta hivyo vitafutwa.
Akitangaza kufunguliwa kwa minada ya ufuta itakayoanza jumamosi ijayo ya tarehe 11 Juni 2022 amewataka wakulima kutouza ufuta wao nje ya mfumo rasmi (kangomba) na badala yake wasubiri kuuza kupitia mfumo rasmi ambao kwa msimu huu bei ya ununuzi wa ufuta ni nzuri sana.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.