Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab R. Telack akizungumza na viongozi wa kamati ya dini mbalimbali za Mkoa wa Lindi jana amewaomba viongozi hao kufanya ibada maalum ya kuuombea Mkoa wa Lindi.
Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema hayo kutokana na majanga mbalimbali yanayouandama Mkoa wa Lindi hivyo tuone haja ya kumkimbilia mwenyezi mungu ili atuondolee ugonjwa unaosumbua nchi na dunia kwa ujumla wa UVIKO-19. Amewaomba pia viongozi hao kuwa mstari wa mbele na kuwaelekeza waamini wao kuchukua tahadhari zote zinazoelekezwa na serikali juu ya kujikinga na ugonjwa kwenye mazingira yote ikiwemo ya ibada.
Pamoja na maombi hayo, Mhe. Mkuu wa Mkoa amewaomba viongozi hao kupitia ibada hiyo maalum Mkoa wa Lindi uombewe dua/sala maalum ili Mkoa ufunguke na watu waweze kuziona fursa kwa urahisi na kuacha kufanya matendo yasiyofaa. Aliyasema hayo kutokana na vitendo mbalimbali vya uvunjifu wa sheria ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakivifanya mara kwa mara ikiwemo suala la uchomaji moto kwenye mazingira kutokana na imani potofu.
Mhe. Mkuu wa Mkoa akioneshwa kushangazwa na matukio Wilayani Kilwa ya mauaji ya wakulima na wafugaji pamoja na wanakijiji wanaoishi kwenye pori la hifadhi la Miguruwe kuwatekwa askari 17, amewaeleza viongozi hao kuwa hatomvumilia au kumuonea haya mtu yeyote atakayejihusisha na uhalifu hata kama ni mwanamke mjamzito atachukuliwa hatua kali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.