Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab R. Telack leo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sokoine alizindua uchomaji wa chanjo ya kuzuia maambukizi ya ugongwa wa UVIKO-19 kwa Mkoa wa Lindi na amewaeleza wananchi kuwa chanjo hiyo iliyotolewa na Serikali imepitia kwenye mamlaka zote za uhakiki ubora hivyo ina viwango sahihi na ina ubora mzuri. Amewaomba wananchi kutosikiliza maneno ya upotoshaji na badala yake wajitokeze kwa wingi kupatiwa chanjo hii ili wapate kinga kwa ajili ya maisha yao pia amewakumbusha wananchi kwamba kuchoma chanjo ni hiari ya mtu. " Nawasihi kujitokeza kupata chanjo katika vituo vya Hospitali ya Sokoine, Kituo cha Afya cha Mnazi Mmoja, Kituo cha Afya cha Mjini, Kituo cha Afya cha Kitomanga kwa Manispaa chanjo ni chache tuwahi", amesema Mhe. Zainab R. Telack.
Pamoja na maelezo hayo, Mhe. Mkuu wa Mkoa amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Lindi kuwa chanjo zimesambazwa kwenye Wilaya zote za Mkoa wa Lindi na zitatolewa kwenye vituo vilivyotangazwa. Pia amewaomba viongozi wa dini, Serikali na taasisi mbalimbali kuwaeleza wananchi kuhusu kuchukua tahadhari zote kwa kunawa mikono na sabuni, kuvaa barakoa, kufanya mazoezi na kuepuka misongamano isiyokuwa ya lazima.
Dawa ya chanjo imetolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Mikoa ya yote baada ya uzinduzi wa kitaifa uliofanywa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 28 Julai 2021 ikiwa ni jitihada ya kupambana na ugonjwa hatari wa UVIKO -19 unaoisumbua nchi na dunia kwa ujumla.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.