Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab R. Telack amesema hayo leo tarehe 17 Juni 2021 kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi alipokuwa anafungua kikao kazi cha uchambuzi wa mipango na bajeti ya maendeleo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa itakayotekelezwa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri kwa mwaka 2021/2022." Wakurugenzi tufanye kazi, tusikae kusubiri mkeka wa uteuzi" amesema Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Pamoja na kusisitiza suala la utendaji, Mhe. Mkuu wa Mkoa amewataka Maafisa Mipango wa Halmashauri kuwashauri wakurugenzi vizuri, na wakurugenzi wahakikishe wanazifahamu Halmashauri zao vizuri kwa maslahi mapana ya wengi. Amewaeleza wakurugenzi na Maafisa Mipango katika ziara yake ya muda mfupi aliyofanya amejionea changamoto ya ubovu wa barabara nyingi ambazo hazipitiki, jambo ambalo linaadhiri ushawishi kwa wawekezaji. Hivyo, Kupitia kikao kazi hicho amewataka itengwe bajeti ya kuchonga barabara zenye changamoto za kutopitika.
Katika mipango iliyoainishwa, Mhe. Mkuu wa Mkoa kwa msisitizo mkubwa amewaeleza watendaji wa Halmashauri hatokubali kuona 10% ya fedha zinazotengwa kupitia bajeti kwa ajili ya maendeleo ya kina mama, vijana na walemavu haziwanufaishi wahusika. Aliongezea kuwa kutotekeleza uwezeshaji wa makundi hayo kwa 100% ni kumuangusha Mhe. Rais, kitendo ambacho hakikubaliki. Sambamba na hilo amewataka wakurugenzi wawasilishe fedha za lishe za watoto wa shule kwa 100% na wakati husika.
Mhe. Mkuu wa Mkoa amezielekeza Halmashauri zote kupitia 10% ya fedha zinazotengwa kwa kina mama, vijana na walemavu vinunuliwe vifaa vya vikundi husika badala ya kuwapatia pesa taslimu kitendo kinachokwamisha malengo ya vikundi mbalimbali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.