Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi leo tarehe 6/4/2017 amepokea msaada wa mashuka 50 toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa PSPF akiwakilishwa na Meneja wa PSPF Mkoa wa Lindi Ndg. Mtumwa.
Mashuka hayo yametolewa kwa ajili ya kutumika katika Wodi Daraja la Kwanza katika Hospitali ya Rufaa ya Sokoine ambayo kwa sasa inaendelea kukamilishwa katika ukarabati unaoendelea,
Akishukuru kwa msaada huo, Mhe. Zambi alisema kuwa kitendo walichokifanya PSPF ni njia moja wapo ya Taasisi hiyo kutoa huduma kwa wateja wake kwani nao huugua. “Mkoa peke yake hauwezi kumaliza matatizo yote yaliyopo katika Hospitali ya Sokoine hivyo namshukuru Mkurugenzi Mkuu wa PSPF kwa msaada huu” alisema Mhe. Zambi.
Aidha, amewaomba kuto kuuchoka Mkoa pale utakapoomba misaada mingine kwani changamoto bado zipo nyingi. Pia ameziomba taasisi nyingine nazo kujitoa katika kusaidia Mkoa kukabiliana na changamoto zilizopo.
Katika makabidhiano hayo alikuwepo Katibu Tawala Mkoa, Ndg. Ramadhan Kaswa, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa, Dr. Hussein Athumani na Ndg. Mwanaisha Waziri kutoka PSPF Makao Makuu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.