Mkoa wa Lindi ulibuni utaratibu wa Utoaji tuzo za Elimu kwa Mitiani na pimaji za Kitaifa tangu mwaka 2019 ikiwa ni namna ya kupongezana, kuongeza ushindani, hamasa na motisha miongoni mwa wanafunzi, walimu, wasimamizi wa sekta na idara mbalimbali za elimu na wanajamii kwa ujumla.
Hayo yameelezwa na Katibu Tawala Msaidizi Elimu Mkoa wa Lindi Mwalimu. Joseph Mabeyo wakati akitoa taarifa ya hali ya elimu katika hafla ya utoaji wa tuzo za elimu kwa shule, walimu,wanafunzi na Halmashauri zilizofanya vizuri katika mitiani na pimaji za kitaifa zilizofanyika mwaka 2024 pamoja na Uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Elimu Mkoa wa Lindi, ambapo kwa mwaka huu hafla hizo zimefanyika wilayani Ruangwa.
Katika hafla hiyo inayokwenda na Kauli Mbiu isemayo 'Uwajibikaji Wangu ni Msingi Mwl. Mabeyo amewapongeza walimu na wanafunzi sambamba na ushirikiano wa wazazi na mshikamano ambao umechagiza kupatikana kwa matokeo chanya kwa kuongeza ufaulu kimadaraja na kuendelea kupunguza idadi ya wanafunzi wanaopata daraja sifuri kutoka wanafunzi 375 mwaka 2023 hadi 335 sawa na 4.16% mwaka 2024.
Aidha, kwa kuzingatia kuwa sekta ya Elimu ndio msingi wa ustawi wa Mkoa wa Lindi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla, Mwl. Mabeyo ameeleza kuwa Mkoa utaendelea kufanya tathmini ya Mpango Mkakati wa Elimu inayowekwa kila mwaka na kuendelea kutoa tuzo za Elimu kwa walimu na wanafunzi ili kuzidi kujenga ari ya kujituma zaidi na kuzidi kupata matokeo chanya
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.