• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

MILIONI 565 ZATOLEWA KWA VIKUNDI 136 MIKOPO YA 10% HALMASHAURI YA WILAYA RUANGWA

Posted on: February 10th, 2025

ZAIDI YA MILIONI 565 ZATOLEWA KWA VIKUNDI 136 VYA WANAWAKE,

Shilingi Milioni 565,517,154/= zimetolewa kwa vikundi 136 vya Wanawake, Vijana, na Watu wenye Ulemavu kupitia mpango wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, hafla ya uzinduzi wa mikopo hiyo imefanyika leo, Februari 7, 2025, katika ukumbi wa hoteli ya Ruangwa Pride, ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe. Hassan Ngoma, kwa kushirikiana na uongozi wa Halmashauri hiyo.

Mhe. Ngoma ameagiza viongozi wa Wilaya na Halmashauri kuhakikisha kuwa kanuni za utoaji mikopo zinazingatiwa, mikopo inasambazwa kwa haki na kwa wakati, ili kufanikisha lengo la Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, la kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Ndugu Frank Komba, amesema kuwa kati ya vikundi vilivyonufaika, 78 ni vya Wanawake, 48 vya Vijana, na 10 vya Watu wenye Ulemavu. Ameeleza kuwa ufuatiliaji na usimamizi wa mikopo hiyo unapaswa kuimarishwa ili kuhakikisha marejesho yanafanyika kwa wakati na kuwapa fursa wengine kunufaika.

Naye, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mhe. Andrew Chikongwe, amewataka wanufaika kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa na kuhakikisha wanarejesha kwa wakati, lakini pia, amesisitiza umuhimu wa wanavikundi kushiriki katika shughuli za kijamii na maendeleo, ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mikutano ya hadhara.

Kwa upande wao, wanufaika wa mikopo hiyo, akiwemo Rehema Saidi, mwakilishi wa vikundi vya Wanawake, Kasimu Mnanguka kutoka Kikundi cha Mshikamano mwakilishi wa vijana, na Ramadhan Abdallah, mwakilishi wa Watu wenye Ulemavu, wameishukuru Serikali kwa kuwawezesha na wameahidi kurejesha mikopo kwa wakati ili kusaidia wengine kunufaika.

Ili kuhakikisha mpango huu unaleta matokeo chanya, ni muhimu kwa wanufaika kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa na kuimarisha nidhamu ya marejesho.

@lindi_rs_

7 February

lindi_rs_'s profile picture

Post

ruangwadc's profile pictureruangwadc•

  • Photo shared by Halmashauri Ya Wilaya Ruangwa on February 07, 2025 tagging @lindi_rs_. Inaweza kuwa picha ya Watu 6, bango, bango na maandishi yanayosema 'HALMASHAURI YA WILAYA YA RUAN HAFLA YA UZINDUZI WA UTOAJI WA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJ WAT ATOWENYE VENYE EMAVU TS 565, CRDB BANK K bank nkE thatIistens hat UPA PAY TASHIMU. DATE 07/02/2025 07/02/ 2025 MILIONI MiA TANO SHILLINGS SHILLINGS CAUACIZO| kumi SABA ELFU, MIA ทหตัค IT2I NA' TANO, MIA 해티 PAETZS 565,517,1 565 154/ HAmSINI NNE Tu. TAFADILALIUSIANDIKEGHINI IANDIKECHINIY AMSTARIT STARIHUJ HUJ 11100 AUTHGRISED SIGNATURE 79-032581= 1087112000 11'.

    lindi_rs_

  • Photo by Halmashauri Ya Wilaya Ruangwa on February 07, 2025. Inaweza kuwa picha ya Watu 2, jukwaa na maandishi.

41 likes
ruangwadc 

ZAIDI YA MILIONI 565 ZATOLEWA KWA VIKUNDI 136 VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU

Shilingi Milioni 565,517,154/= zimetolewa kwa vikundi 136 vya Wanawake, Vijana, na Watu wenye Ulemavu kupitia mpango wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, hafla ya uzinduzi wa mikopo hiyo imefanyika leo, Februari 7, 2025, katika ukumbi wa hoteli ya Ruangwa Pride, ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe. Hassan Ngoma, kwa kushirikiana na uongozi wa Halmashauri hiyo.

Mhe. Ngoma ameagiza viongozi wa Wilaya na Halmashauri kuhakikisha kuwa kanuni za utoaji mikopo zinazingatiwa, mikopo inasambazwa kwa haki na kwa wakati, ili kufanikisha lengo la Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, la kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Ndugu Frank Komba, amesema kuwa kati ya vikundi vilivyonufaika, 78 ni vya Wanawake, 48 vya Vijana, na 10 vya Watu wenye Ulemavu. Ameeleza kuwa ufuatiliaji na usimamizi wa mikopo hiyo unapaswa kuimarishwa ili kuhakikisha marejesho yanafanyika kwa wakati na kuwapa fursa wengine kunufaika.

Naye, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mhe. Andrew Chikongwe, amewataka wanufaika kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa na kuhakikisha wanarejesha kwa wakati, lakini pia, amesisitiza umuhimu wa wanavikundi kushiriki katika shughuli za kijamii na maendeleo, ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mikutano ya hadhara.

Kwa upande wao, wanufaika wa mikopo hiyo, akiwemo Rehema Saidi, mwakilishi wa vikundi vya Wanawake, Kasimu Mnanguka kutoka Kikundi cha Mshikamano mwakilishi wa vijana, na Ramadhan Abdallah, mwakilishi wa Watu wenye Ulemavu, wameishukuru Serikali kwa kuwawezesha na wameahidi kurejesha mikopo kwa wakati ili kusaidia wengine kunufaika.

Ili kuhakikisha mpango huu unaleta matokeo chanya, ni muhimu kwa wanufaika kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa na kuimarisha nidhamu ya marejesho.

@lindi_rs_

7 February

lindi_rs_'s profile picture

Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • JAMII NA WAZAZI WATAKIA KURUDI KUBEBA JUKUMU LA MALEZI KWA WATOTO

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA WA LINDI AONGOZA KIKAO CHA LISHE NGAZI YA MKOA

    May 03, 2025
  • MHE. TELACK AZINDUA MPANGO MKAKATI WA ELIMU MKOA WA LINDI KWA MWAKA 2025

    May 02, 2025
  • RC TELACK AKABIDHI TUZO ZA ELIMU KWA WALIMU,WANAFUNZI NA HALMASHAURI ZILIZOFANYA VIZURI MKOANI LINDI.

    May 02, 2025
  • tazama zote

Video

CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA CHAMA CHAO MAPEMA ILI KUWAPA UTULIVU WANACHAMA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO ILI WANACHAMA WAPATE UTULIVU

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.