Hayo yamebainika katika uzinduzi wa Kampeni ya upandaji miti Kimkoa Kwa mwaka 2022/23 iliyofanyika Jumatano ya tarehe 19 Aprili 2023 katika Shule ya Wasichana iliyopo katika kata ya Kilangala, Manispaa ya Lindi.
Akizindua Kampeni hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga amesema kuwa Mkoa wa Lindi unashika namba mbili kwa kuwa na misitu mikubwa ya asili iliyotunzwa vizuri, huku Mkoa wa Katavi ukishika namba moja.
Mhe. Ndemanga ameongeza kuwa ili kuendelea kuhifadhi misitu yetu ni lazima kila taasisi, kijiji, Kata, Wilaya ihakikishe inapanda miti katika maeneo yao. Mhe. Ndemanga amewasihi wananchi kuwa wazalendo kwa kutunza Mazingira kwa ajili ya kizazi kijacho.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Christopher Ngubiagai amewasihi wananchi wa Mkoa wa Lindi kutunza Mazingira na misitu vizuri ili iendelee kuchangia mahitaji mahimu kwa maisha ya binadamu na viumbe hai wengine.
Ameongeza kuwa kwa upande wa Wilaya ya Kilwa katika kijiji cha Nanjilinji, misitu imekuwa na faida kubwa kwa jamii ya kijiji hicho. Halmashauri ya kijiji hicho iliwahi kutenga kiasi cha fedha Kwa ajili ya kuwahudumia kina mama wajawazito wote kuanzia hatua ya ujauzito mpaka hatua ya kujifungua.
Mhe. Ngubiagai ameendelea kusema kuwa faida hizi zote zilizopatikana katika kijiji cha Nanjilinji ilitokana na faida iliyopatikana kutokana na mauzo ya mazao ya msitu wa Nanjilinji unaotunzwa na kusimamia na kijiji hicho.
Pamoja na faida hizi, Mhe. Ngubiagai ametoa wito kwa taasisi zote kushikamana na kukabiliana na changamoto zinazochangia kuharibu mazingira ikiwemo kilimo cha kuhama hama cha ufuta, ufugaji usiofuata utaratibu pamoja na uchonaji moto holela.
Katika makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru Kati ya Mkoa wa Lindi na Ruvuma, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndg. Abdalla Shaib Kaim akizungumza na wananchi katika kijiji cha Sautimoja, Wilaya ya Tunduru alisema kuwa amefurahishwa Sana na mazingira ya kijani ya Mkoa wa Lindi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.