Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack Jana Jumatano amekutana na viongozi na watendaji wa Shirika la Mafuta Tanzania, TPDC, Makampuni ya gesi na Mafuta Equinor na Shell, pamoja na Kampuni ya Ushauri na Usimamizi wa Miradi, RSK Tanzania.
Wataalam hao wamefika Leo Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kutambulisha mradi wa kilimo, mifugo, uvuvi, miundombinu na biashara utakaolenga jamii iliyohamishwa eneo la Likong'o, Manispaa ya Lindi kupisha utekelezaji wa mradi wa gesi, LNG.
Mkurugenzi wa Kampuni ya ushauri na Usimamizi wa Miradi, RSK Tanzania Ndg. Jesper Bosse Jonsson amesema kuwa lengo kuu la mradi huu ni kurudisha hali ya uchumi ya jamii iliyohamishwa kutoka eneo hilo la mradi wa gesi. Ameongeza kuwa mradi huu wa miaka mitatu utaanza kwa kuwatambua walengwa na kutambua mahitaji yao kwenye shughuli za kilimo, mifugo, Uvuvi, biashara na miundombinu.
Mhe. Telack amewataka watekelezaji wa mradi huo kuzingatia mahitaji halisi ya walengwa ikiwemo wavuvi na shughuli zao za Uvuvi, wakulima, maeneo yao ya uzalishaji na wengine.
Mhe. Telack Amesisitiza kuwa mradi huo utekelezwe kikamilifu na uwafikie walengwa wote bila kumuacha mnufaika hata mmoja.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.