Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack, jumamosi ya tarehe 09 Machi 2024 ameongeza kikao Kwa kwanza cha maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kukimbizwa Mkoani Lindi kuanzia tarehe 24 Mei 2024.
Kupitia kikao hicho Mhe. Telack amewataka viongozi wote kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya mbio hizo huku akizisisitiza Halmashauri zote za Mkoa wa Lindi kuandaa miradi mizuri iliyotekelezwa kwa kiwango bora.
Ameongeza kuwa Mkoa wa Lindi umepokea fedha nyingi za utekelezaji wa miradi mbalimbali katika sekta ya afya, maji, miundombinu, uwezeshaji jamii na maeneo mengine hivyo miradi ipo mingi na yenye vigezo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.