Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack ametoa agizo la kufanya msako mkali kwa wazazi na walezi wote ambao wameshindwa kuwapeleka watoto wao ambao wamechaguliwa kujiunga kuanza masomo yao ya kidato cha kwanza kwa muhula mpya wa masmo kwa mwaka 2023.
Mhe. Telack ametoa agizo hilo kufuatia kutoridhishwa na hali ya mahudhurio ya wanafunzi wanaopaswa kujiunga na masomo ya sekondari katika shule ya sekondari Mikoma, iliyopo katika kata ya Pande, wilaya ya Kilwa ambapo pia amegaazia watendaji wa kata kuandaa mkataba maalumu ambapo mzazi atatakiwa kuhaidi kumsimamia mtoto wake kusoma hadi atakapomaliza bila utoro wala kukatisha masomo.
“Tutatembea na polisi hapa, tutatembea na mahakama inayotembea pia, tukimkuta mzazi hajapeleka mtoto wake shule hukumu itatoka hapohapo, sasa ili tusifike huko watoto wapelekwe shule, tuachane na visingizio vya watoto hawana sare, wavae zile walizokuwa wanavaa shule za msingi hayo ndio maelekezo ya serikali ili tu asibakie mtoto ambaye hajaenda shule wakati wenzao wameshaanza masomo, hawa walimu wetu hawatarudi nyuma kufundisha na wala siku za kukaa darasani hazitaongezwa kwakua mtoto wako hajaripoti shuleni. Natoa siku saba tu walimu wakuu watuambie idadi ya watoto ambao bado hawajaripoti shuleni ili tuanze msako nyumba hadi nyumba”
Mkuu wa shule ya Mikoma, Mwalimu Julius Peter ameeleza “ Kwa mwaka 2023, tunapaswa kuwa na wanafunzi 113, ambao kati yao wavulana ni 40 na wasichana 73 lakini hadi sasa wanafunzi walioripoti shuleni kwa ajiri ya kuanza masomo yao jumla yao ni 37 wakiwemo wavulana 17 na wasichana 20 huku wanafunzi 76 wakiwa bado hawajaripoti shuleni na masomo tayari yameshaanza”
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.