Hayo yamesisitizwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack wakati anaongoza kikao cha utoaji wa elimu juu ya mafanikio ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2000 inayoishia 2025 pamoja na maandalizi ya uandaaji wa Dira mpya itakayotekelezwa mpaka kufikia 2050.
Katika kikao hicho kilichofanyika jana alhamisi, ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mhe. Telack amewasisitiza Viongozi wa Mkoa wa Lindi kutoa elimu kwa wananchi katika zoezi linalotarajiwa kufanyika la ukusanyaji wa maoni yatakayofanikisha uandaaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya miaka 25 mpaka kufikia 2050.
Awali akizungumza na wajumbe wa kikao, Dkt. Crispin Ryakitimbo ambaye ni mjumbe wa sekretariet ya maandalizi ya uandaaji wa Dira ya Taifa 2050 amesema kuwa kwa sasa maandalizi ya uandaaji wa Dira ya Maendeleo ya 2050 yameanza kufanyika wakati huu ambao Dira ya Taifa ya mwaka 2025 inaenda kufikia mwisho.
Dkt. Ryakitimbo ameeleza kuwa kuelekea utekelezaji wa zoezi la uandaaji wa Dira ya Taifa ya miaka 25 itakayoishia mwaka 2050, wananchi watashiriki kutoa maoni kwa kutumia njia mbalimbali zitakazowezesha zoezi hilo kufanikiwa.
Ameongeza kuwa maoni yatatolewa na wananchi wenye umri kuanzia miaka 15 ambapo njia tofauti tofauti zitatumika kama vile mikutano ya hadhara, majadiliano, simu, ujazaji wa madodoso na zingine ambazo zitaonekana zinafaa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan Ngoma amewataka wananchi kushiriki kikamilifu kwenye uandaaji wa Dira hii ya mwaka 2050 kwa kuwa ndiyo inayotoa mwelekeo wa maisha kwa kila mwananchi kwa kipindi cha miaka 25.
Hivyo, Mhe. Ngoma amewataka wananchi wote hasa vijana kujitokeza ili kufanikisha zoezi hili ambalo ni muhimu kwa maendeleo ya elimu, kilimo, madini na sekta zote za uchumi, jamii na siasa.
Sekretariet ya Maandalizi ya Dira ya Taifa 2050 imeanza zoezi la majaribio katika baadhi ya mikoa ikiwemo ambapo kwa Mkoa wa Lindi itakusanya maoni ya Viongozi na wananchi katika Halmashauri ya Ruangwa na Manispaa ya Lindi.
ReplyForward |
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.