Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack ameyasema hayo katika kikao Kati ya uongozi wa Mkoa, timu ya afya ya Mkoa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Madaktari wasio na mipaka, Medecins Sans Frontiers ndg. Stephen Cornich kilichofanyika Jana jumatano, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Telack amemuomba Mkurugenzi Cornich kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha huduma za afya kwa Mkoa wa Lindi.
Mhe. Telack ameeleza eneo ambalo linahitaji nguvu kubwa ni mafunzo kwa vitendo ambayo yataongeza uwezo wa kitaalam kwa madaktari na watoa huduma za afya kwa ujumla.
Pamoja na mafunzo, pia amemuomba Mkurugenzi huyo kuongeza wataalam wa afya ambao watashirikiana na wataalam wa Serikali kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wa Lindi.
Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi Dkt. Khery Kagya amesema kuwa Shirika lisilo la kiserikali, Medecins Sans Frontiers lenye makao yake makuu Geneva, uswizi katika Wilaya ya Liwale limeendelea kusaidia katika maeneo ya huduma ya afya ya mama na mtoto.
Ameongeza kuwa katika Wilaya ya Liwale huduma ya afya ya mama na mtoto inatolewa kupitia vituo vya afya Saba ikiwemo Hospitali ya Wilaya, vituo vya afya viwili na zahanati nne.
Akizungumza na vyombo vya habari, Mkurugenzi Mkuu wa Medecins Sans Frontiers, Ndg. Stephen Cornich amesema kuwa amefika nchini Tanzania kutokea Uswizi kwa ajili ya kujionea namna ambavyo huduma ya afya ya mama na mtoto ilivyoboreshwa katika Wilaya ya Liwale.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.