KWA UFUPI
Mradi wa kusindika gesi asilia, LNG kuanza kazi Mkoani Lindi. Hayo yamesemwa leo Novemba 13, 2020 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr John Pombe Magufuli katika hotuba yake wakati akizindua bunge la 12 jijini Dodoma. Amesema pia Serikali itahamasisha matumizi ya gesi asilia na gesi ya mitungi katika matumizi ya nyumbani, taasisi, viwandani pamoja na magari.
"kwenye miaka mitano ijayo, tutaanza utekelezaji wa Miradi ya kielelezo (flagship projects) ya Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga lenye urefu wa kilometa 1,445 pamoja na Mradi wa Kusindika Gesi Asilia (LNG) Mkoani Lindi. Zaidi ya hapo, tutaendelea kuhamasisha matumizi ya gesi asilia na gesi ya mitungi majumbani, kwenye taasisi, viwanda na magari ili kupunguza uharibifu wa mazingira na athari za mabadiliko ya tabianchi," Amesema Mhe. Rais.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.