Kuelekea simu mpya wa ununuzi wa zao la ufuta mwaka 2025, Mkoa wa Lindi unatarajia kuzalisha na kuuza kg 78,189,500 za ufuta kulingana na hali ya hewa ya mwaka huu.
Kati ya kiasi hicho ,Chama kikuu cha ushirika cha Lindi Mwambao inakusudia kukusanya na kuuza kg 43,987,00 na Runali 34,202,500.
Aidha, maghala yanatarajiwa kufunguliwa kuanzia juni 1,2025 huku minada ikitarajiwa kuanza wikiendi inayofuata kutegemea na mzigo utakaokuwa umekusanywa kwenye maghala makuu.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, leo Mei 22,2025 akiwa kwenye kikao cha maandalizi ya ununuzi wa zao hilo ameendelea kuhimiza vyama vya ushirika na viongozi wa serikali kuhakikisha wanasimamia ubora wa zao hilo ili minada ikafanyike kwa ufanisi na wakulima wapate bei nzuri.
Akieleza hali ya uzalishaji wa zao la ufuta Katibu Tawala Msaidizi, uchumi na uzalishaji Mwinjuma Mkungu amesema wakala wa vipimo kwa kushirikiana na kampuni ya Rotai tayari wameshapitia na kuhakiki mizani zote za kidigitali zitakazotumika kupima zao la ufuta.
Sambamba na hilo ameeleza kwamba kwa misimu mitano mfululizo hali ya uzalishaji wa zao la ufuta kwa Mkoa wa Lindi umekuwa ukiimarika zaidi tofauti na misimu ya nyuma ikiwa ni kutokana na matumizi ya mfumo rasmi wa mauzo ambao umeleta tija na bei shindani kwa wanunuzi na kumnufaisha mkulima na Taifa kwa ujumla.
@ushirika_tcdc
@wizara_ya_kilimo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.