Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dustan Kitandula ameeleza moja ya mkakati wa haraka ambao unakwenda kutekelezwa na serikali katika kukabiliana na mnyama Ndovu ambao wanavamia makazi ya wananchi katika jimbo la Mchinga na Mtama ni kupeleka mabomu baridi 1000 ambayo yameonesha ufanisi katika zoezi la kuwafukuza Tembo.MLola
”Mhe. Mbunge alisema mwezi wa tano wasita hivi tulifanya zoezi la kukabidhi mabomu baridi kwaajili ya kuja kufukuza Tembo hii ni kazi kubwa imefanywa ya utafiti kwa taasisi yetu ya TAWA kwa kushirikiana na wenzetu wa Jeshi la Mzinga, watu wetu wa TAWIRI ambao ndiyo wanaohusika na utafiti kwa kuona yale mabomu ya zamani ambayo tulikuwa tunayatumia udhaifu wake ni nini, nini kifanyike kuyaongezea nguvu, nafurahi kusema, sasa tunayo mabomu ambayo yanauwezo mkubwa wa kufukuza Tembo na ndiyo hayo tuliyagawa ya kufanya majaribio. Kwa Lindi, Nachingwea na Liwale tulitoa mabomu karibu 200 sasa kwa safari hii, tunakuja kwa nguvu kubwa zaidi hapa Mchinga Mhe. Mbunge tunakuletea mabomu 500 kwa ndugu yangu Nape tunapelekea mabomu 500 hii katika kuhakikisha zoezi la kufukuza wanyama hawa lifanyike vizuri " Alisema Mhe. Kitandula.
Ameongeza kwakusema katika bajeti hii ya mwaka 2024/2025 imeongezwa bajeti ya kununua helkopata mbili, Ngefe nyuki na kufanya mafunzo kwenye vijiji vyote ambavyo vinachangamoto ya Ndovu ili wananchi wapate elimu ya namna ya kufukuza wanyama hao kwani siyo kila mtu anaweza kufukuza tembo.
Mhe. Kitandula ametuma fursa hiyo kutoa pole na kuwataka wahusika wanaowasilisha taarifa za changamoto zinazotokana na Ndovu kuanzia ngazi ya kata na halmashauri kuharakisha kuwasilisha taarifa pale inapotokea uharibifu wa mazao, kifo au kujeruhiwa kwa ajili ya kutoa kifuta machozi kwa wale wote ambao wamepata changamoto za aina hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack ameeleza kuwa kwasasa Mkoa umejipanga vizuri kuhakikisha hakuna migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo itatokea ndani ya Mkoa, ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha hakauna mfugaji ambaye anaingiza Ng’ombe katika maeneo yao pasipo kibali, yeyote ambaye ataingiza mifugo kinyume na utaratibu hatua zitachukuliwa dhidi yake.
Yameelezwa hayo baada ya kubainika kuwa shughuli mbalimbali za wananchi hasa ufugaji wa Ng’ombe na kilimo cha kuhama hama kuvamia hifadhi na kupelekea Ndovu kuanza kutafuta maeneo mengine ambayo watapata maji na chakula.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.