Mwenyekiti wa kamati ya uratibu wa uchaguzi Mkoa wa Lindi Dkt. Bora Haule mapema leo, amekuwa wa kwanza kujiandikisha katika daftari la mkazi katika kituo cha kujiandikishia Ripsi ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kuweza kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Akizungumza baada ya kujiandikisha, Dkt. Bora ametoa rai kwa wananchi wote wa Mkoa wa Lindi kuhakikisha wanakwenda katika vituo vya kujiandikisha kwa wakati na kusisitiza kuwa kujiandikisha katika daftari la mkazi ni hatua muhimu kwa kila mwananchi kushiriki katika uchaguzi na kutoa sauti yao kwa kuchagua viongozi wa serikali za mitaa ambao wataongoza maendeleo ya jamii zao.
Aidha, Dkt. Bora ameeleza kwamba zoezi la uandikishaji linaendelea vizuri katika vituo vyote 16 alivyovitembelea leo kuanzia saa 1:30 asubui ili kuhakikisha kuwa zoezi la kujiandikisha linakwenda kwa ufanisi na wananchi wanapata huduma stahiki katika vituo vya kujiandikishia vilivyo karibu na maeneo yao.
Zoezi la kujiandikisha katika daftari la Mkazi limeanza rasmi leo katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Lindi na wananchi wanahimizwa kutumia siku zilizobakia kuhakikisha wanajiandikisha ili wasikose nafasi ya kushiriki katika uchaguzi huo muhimu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.