Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema hayo siku ya Jumatatu ya terehe 13 Septemba 2021 alipotembelea na kuzungumza na jamii za wakulima na wafugaji kwenye mikutano miwili iliyofanyika katika vijiji vya Nakiu na Nanjilinji vilivyopo Wilaya ya Kilwa.
Akizungumza wa wananchi hao, Mhe. Abdallal Ulega aliwapa pole kwa vifo vilivyotokea katika vijiji hivyo vilivyotokana na mapigano kati ya wakulima na wafugaji wiki chache zilizopita. Wakioneshwa kuchoshwa na vitendo vya kupigwa mara kwa mara na vyombo vya dola kutotenda haki, wakulima wamemuomba Naibu Waziri kuwaondoa wafugaji na kuwapeleka mahali pengine, “ Wafugaji watafutiwe maeneo mengine ili amani ipatikane ” mkazi wa kijiji cha Nanjilinji ndugu. John Bundala alieleza. Kundi la wafugaji lilieleza mbele ya mkutano sababu zinazopelekea kutokea kwa mapigano makubwa ni viongozi kuchelewa kuchukua hatua pale inapoonekana kuna dalili ndogo ndogo za migogoro, pia kutokuwepo kwa kituo cha Polisi kwenye tarafa nzima ya Nanjilinji.
Mhe. Abdallal Ulega amezitaka jamii zote mbili kuishi kwa amani, kuthaminiana na kutambua umuhimu wa shughuli za jamii moja na nyingine kwa kuwa maisha ya jamii zote mbili ni kutegemeana. Akioneshwa kutofurahisha na migogoro ya wakulima na wafugaji amewataka viongozi wa vijiji, kata, tarafa na wilaya kuchukua hatua haraka pindi zinapojitokeza dalili za vurugu. Pia amewataka viongozi hao kuunda kamati za amani na maridhiano sambamba na kuunda njia za kupita ng’ombe wanapoelekea kunywa maji kwenye mto wa mbwemkulu ili kuepusha uharibifu wa mazao.
Mhe. Abdallal Ulega ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imalize ujenzi wa kituo cha Polisi cha Nanjilinji ili kusogeza huduma ya usalama kwenye maeneo hayo, pamoja na hilo pia amewataka watende haki wanapofanya maamuzi mbali mbali yanayohusisha makundi hayo mawili.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.