Mkuu wa wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi ameyataka Mashirika yasiyo ya kiserikali kutafuta Taarifa Muhimu na kutumia Takwimu Sahihi katika utekelezaji wa majukumu yao.
"Kwahiyo niwasihii sana NGOs za Mkoa wa Lindi tumieni takwimu sahihi kutoka maeneo sahihi, zingatieni sheria " Mhe. Ndemanga.
Ametoa wito huo kwa wajumbe wa NGOs katika kikao cha baraza la wajumbe wa mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka wilaya zote za Mkoa wa Lindi, kilichofanyika ukumbi wa DDC Mjini Lindi .
Amesema Mashirika yasiyo ya kiserikali yanakazi kubwa sana ya kuhakikisha wananchi wanapata taarifa muhumi na sahihi. Ili wananchi waweze kupata taarifa hizo ni wajibu wa NGOs kutembelea miradi au ofisi zenye taarifa husika ikiwemo miradi inayoendelea ndani ya mkoa na changamoto mbalimbali ambazo zinahiyaji kutatuliwa serikali au wqadau wa maendeleo hasa NGOs, kwakufanya hivyo ni wazi jamii itakuwa imepata msaada mkubwa.
Licha ya kupata taarifa hizo ambazo zitawasaidia wananchi bali zitawasaidia hata NGOs zenyewe kuepuka usumbufu wa kisheria hasa itakapobainika kutumika kwa taarifa zisizo sahihi kutoka chanzo ambacho siyo sahihi.
Mhe. Ndemanga ametumia fursa hiyo kuzitaka NGOs kuendelea kutoa hamasa kwa wananchi juu ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi Mkuu hapo mwakani 2024, kwa kujiandaa kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura ambapo zoezi la uwandikishaji linatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.