Ofisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa {TAKUKURU} Mkoa wa Lindi kupitia Programu ya TAKUKURU Rafiki imefanikiwa kutatua Kero ya ardhi iliodumu kwa muda wa takribani miaka tisa iliyokuwa inahusisha Eneo la Chuo cha Ufundi Stadi VETA na Ofisi ya Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Lindi, Bi.Asha Kwariko katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za TAKUKURU Mkoa wa Lindi, leo Machi 23, 2024 ambapo ameeleza kuwa kero hiyo imebainisha kuwa eneo ambalo chuo cha VETA waliomba kumilikishwa na Halmashauri ya Lindi ni dogo kulinganishwa na eneo walilolipa fidia wananchi ili waachie ardhi na kutokutekelezwa kwa mchakato wa kuonyeshwa mipaka ya eneo husika hivyo kuchelewesha mchakato wa Chuo cha VETA kumiliki ardhi.
"Kupitia majadiliano yaliyofanyika baina ya TAKUKURU Lindi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi pamoja na wataalam wake kwa lengo la kupata majawabu, utatuzi wa kero hiyo ulipatikana ambapo VETA Lindi imeonyeshwa mipaka ya ardhi hiyo iliyoombwa kwa ajiri ya matumizi ya chuo hiko. Aidha, Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi ameifahamisha VETA Lindi kuwa eneo hilo ni mali yao na kwa sasa VETA imeanza mchakato wa umiliki wa ardhi hiyo kupitia ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa lindi na kuhusu ukubwa wa eneo walilopewa, majadiliano kati ya Taasisi hizi mbili chini ya uratibu wa TAKUKURU Lindi yanaendelea" ameeleza.
Aidha, TAKUKURU Lindi imeendelea na majukumu yake ya Uzuiaji wa Rushwa kwa kufanya Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika kipindi cha mwezi Januari hadi Machi ambapo jumla ya miradi 12 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 7 kwenye sekta za Elimu, Maji, Kilimo, Uvuvi na Tamisemi na kubaini mapungufu katika miradi mitatu ya Elimu yenye jumla ya Shilingi Bilioni. 1,199,008,654.00 hivyo hatua mbalimbali zilichukuliwa ili kurekeebisha mapungufu hayo.
Vilevile, katika kipindi cha mwezi April hadi Juni 2024, TAKUKURU Lindi imejipanga kuendelea kutekeleza majukumu ya udhibiti vitendo vya Rushwa kwa kufanya ufatiliaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Mkoa wa Lindi, ufuatiliaji wa karibu wa ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri pamoja na ushirikishaji wa wananchi na wadau mbalimbali katika maeneo ya ushirikiano.
"Sambamba na hilo, tutaendelea kuchukua hatua stahiki kwa wale wote watakaobainika kufuja mali za umma, na kjwa kushirikiana na ofisi ya Taifa ya Mashtaka tutawafikisha mahakamani watuhumiwa wa vitendo vya Rushwa. Aidha, tutaendelea kutilia mkazo na kuongeza juhudi kwa kuhamasisha ushiriki wa wananchi kupitia nyenzo mbalimbali za uelimishajiumma, kufanya warsha na kuziendeleza klabu za kupambana na Rushwa mashuleni na vyuoni. Kupitia programu ya TAKUKURU Rafiki tutaendelea kuwashirikisha wananchi ambao ni wanufaika wa huduma zetu kutambua kero ambazo zikiachwa bila kupatiwa ufumbuzi zinaweza kusababisha mianya ya vitendo vya rushwa"
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.