Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo leo akiwahutubia wananchi kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika Mkoani Lindi katika uwanja wa michezo Ilulu, Manispaa ya Lindi.
Mhe. Rais amesema kuwa pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana wa washirika wa maendeleo mbalimbali katika kupambana na UKIMWI bado changamoto ya unyanyapaa kwa waadhirika haijafanyiwa kazi vizuri . Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kwa sasa kuna mkakati wa tatu wa kitaifa wa kupambana na janga la UKIMWI ambao utasaidia kuondoa unyanyapaa kwa waadhirika.
“Kuna jambo ambalo hatujalifanyia vizuri, nalo ni suala zima la unyanyapaa, bado lipo na ndio maana tumekuja na mikakati hiyo ili kuondosha huo unyanyapaa.”
“Safari tunayokwenda katika mkakati unaofuata ni kufikia malengo ya sifuri 3 ifikapo mwaka 2030 lakini kwa mpango wetu ni 2026 ni kutokomeza UKIMWI kwa kuwa na sifuri ya maambukizi mapya ya VVU, sifuri ya kifo na sifuri ya unyanyapaa.”
Mhe. Rais amesisitiza kuwa katika kufikia malengo ya kutekeleza wa mpango huu wa miaka 5 ni vyema kushirikiana kwa kuwa mpango huu ni wa sekta zote, sio mpango wa Wizara ya Afya pekee. Mhe. Samia ameilekeza Wizara ya Afya, TACAIDS kwa kushirikiana na sekta zote na wadau wote wa mapambano dhidi ya UKIMWI na VVU kuweka mkazo zaidi katika kuweka jitihada na mikakati madhubuti katika kuzuia maambukizi mapya, kuimarisha huduma za upimaji VVU na matumizi ya ARV ili kutokomeza vifo vitokanavyo na UKIMWI, kuweka mikakati ya kutokomeza ubaguzi na unyanyapaa kwa waadhirika, WAVIU.
Akimkaribisha Mhe. Rais kuzungumza na wananchi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa jitihada mbalimbali zimeendelea kufanyika katika mapambano dhidi ya UKIMWI. Mhe. Majaliwa amesema katika kupambana na janga la UKIMWI mikakati mitatu imeendelea kutekelezwa, kwanza ni pamoja na utafiti wa viashiria vya hali ya VVU hapa nchini ambao ulizinduliwa mwezi septemba 2022. Ameongeza kuwa utafiti huu hufanyika kila baada ya miaka minne ambao utamalizika mwaka 2022/23 ukilenga kupima magongwa ya VVU, homa ya ini B na C. Mkakati wa pili ni mkakati wa tatu wa taifa wa kuthibiti UKIMWI ambao utajuisha sekta zote, na tatu ni mfuko wa udhamini wa udhibiti UKIMWI ambao utakuwa na vyanzo endelevu ili kuhakikisha serikali inakuwa na mchango mkubwa katika kuboresha afua za sekta zote katika kudhibiti VVU na UKIMWI.
Akitoa salam za Wizara ya Afya kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu (Mb), Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Godwin Mollel (Mb) ameeleza hali ya maambukizi kwa nchi nzima kuwa Tanzania inakadiliwa kuwa na waadhirika milioni 1.7 na jumla ya waadhirika milioni moja laki tano na thelathini wamekwisha fikiwa na kupatiwa huduma. Ameongeza kuwa jitihada zinaendelea mpaka kufikia 2026 lengo la kufikia 95,95,95 litatimia. i.e 95 ya kwanza ni kuwafikia waathirika, 95 ya pili ni kuhakikisha wanatumia dawa za kufubaza VVU na 95 ya tatu, waathirika wawe wamefubaza VVU. Mhe. Molle amesema mpaka sasa 92.5% ya waathirika wote wamekwisha fikiwa, 98.3% wamekwisha pata dawa za kufubaza VVU na 97% wamefubaza VVU.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amemshukuru Mhe. Rais kwa kuupatia Mkoa wa Lindi fursa kubwa ya kuwa mwenyeji wa Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kwa mwaka 2022. Mhe. Telack pamoja na shukrani hizo amemshukuru pia Mhe. Rais kwa kuupatia Mkoa wa Lindi jumla ya Tsh. Bilioni 26.8 kwa ajili ya kujenga na kuimarisha miundombinu na huduma za afya, kununua vifaa tiba na dawa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.