Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Ndg. Ngusa Samike ameendelea na ukaguzi wa ujenzi wa kituo cha afya Kipindimbi, wilaya ya Kilwa, kama alivyohaidi kwa wananchi wa eneo hilo ambapo ameridhishwa na kasi ya umaliziaji wa majengo ya awali ya kituo hiko.
“Hapa watumishi naomba tuendelee kuwajibika hasa mhandisi na afisa manunuzi, tuhakikishe tunaleta vifaa eneo la ujenzi kwa wakati visicheleweshe ili huu mradi uanze kutoa huduma, lakini pia tuhakikishe ubora wa haya majengo unaendana na thamani ya fedha iliyotumika hapa na hii inahusisha na ujenzi wa majengo haya mapya ambayo fedha yake imepokelewa na tunatakiwa kujenga jengo la wazazi, jengo la kufulia na jengo la upasuaji, niagize fedha hizi zitumike kwa usahihi na zikamilishe majengo yote kwa kufata maagizo tuliyopewa zile hadithi za kupanda kwa gharama za ujenzi zisiwepo tena kinyume chake ni tutachukuliana hatua”
Pia, Katibu Tawala Mkoa amemuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya kuanza kuandaa mazingira ya kituo kuanza kutoa huduma punde tu watakapokabidhiwa.
“DMO, anza kuandaa mazingira ya upatikanaji wa vifaa tiba, madawa pamoja na watumishi watakaokuja kutoa huduma hapa ili mradi ukikamilika hapa tuanze kutoa huduma za afya kwa wananchi na sio kuanza tena kusubiri kwa muda mwingine wakati wananchi wanahitaji huduma hizo, hivyo tuanze kutoa huduma wakati tun asubiri kukamilika kwa majengo mengine mapya ambayo tushapokea fedha zake na tumeshaanza ujenzi”
Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Ndg. Ngusa Samike anafanya ziara ya kukagua na kufanya tathmini ya huduma za afya ikiwemo kukagua upatikanaji, uhifadhi na msawazo wa madawa pamoja na vifaa tiba katika vituo vya afya,ukusanyaji wa mapato na matumizi ya 50% ya mapato katika vituo vya afya, ukaguzi wa maabara na vipimo vinavyopatikana, utoaji na uhifadhi wa chanjo pamoja na huduma za mama na motto, huduma wa watu waishio na maambukizi ya VVU/UKIMWI pamoja na ukaguzi wa miradi ya afya iliyopo katika halmshauri zote mkoani Lindi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.