Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Ndg. Ngusa Samike amefanya ziara ya ukaguzi katika vituo vya afya katika wilaya ya Kilwa kwa lengo la kufanya tathmini ya huduma za afya katika vituo vya afya, ukusanyaji na utumiaji wa mapato katika vituo vya afya pamoja na upatikanaji wa msawazo wa madawa na vifaatiba katika vituo vya afya ndani ya wilaya hiyo.
Katika ziara hiyo, Katibu Tawala amegundua kukosekana kwa daftari la vihatarishi vya wajawazito pamoja na vipimo vya magonjwa kama kaswende na vidonge vya kuongeza damu kwa wajawazito katika vituo vingi vya afya ikiwemo kituo cha afya Tingi na Kilwa Masoko na kuwataka wafamasia kuhakikisha kunakua na mgawanyo sawa wa madawa na vifaatiba.
“Vipimo kama vya kaswende na dawa za kuongeza damu ni vitu vya umuhimu kwa mama mjamzito kuvipata, sasa unaweza kukuta hapa havipo lakini vituo vingine vipo lakini mahitaji yake ni madogo ukilinganisha na hapa, na hii inapelekea madawa yanaisha wakati wake maana yalipo hakuna watumiaji, lakini pia waganga wafawidhi mjitahidi kufanya maoteo ya madawa na vifaatiba ili kabla havijaisha kabisa katika vituo vyenu muwe mnafahamu hadi lini vitaweza kukidhi na kabla havijaisha muwe tayari mshaomba vingine” Katibu Tawala.
Mganga Mkuu wa Mkoa, Dokta. Kheri Kagya amewaagiza watumishi wa afya wilayani Kilwa kuhakikisha wanaweka kumbukumbu sahihi za dawa zinazotoka na kuingia katika bohari za dawa za vituo vyao pamoja na matumizi sahihi ya mfumo wa GoT -HoMIS na kuhakikisha wanatumia 50% ya mapato kwa kununua madawa na vifaatiba.
“Mfamasia wa wilaya uwe na mazoea ya kutembelea hivi vituo vya afya ili ukague na utoe elimu ya jinsi ya kuhifadhi, utoaji wa dawa na uwekaji wa kumbukumbu wakati wa kupokea na kutoa dawa, wafamasia mliopo vituoni muache tabia ya kujifungia kwenye bogari za dawa huku mnaweza kukaa hata siku mbili tu za wiki kwa ajiri ya kujaza kumbukumbu zenu siku nyingine za wilki mukakae kwenye maduka ya dawa ya vituo muhudumie wananchi, vilevile wajumbe wa CHMT za wilaya maagizo yameshatolewa na nyinyi muwekwe kwenye ratiba za kutoa huduma ili msipoteze ujuzi mlionao katika kutoa huduma za afya hivyo mjiandae kwa hilo” ameongeza Dokta Kagya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.