Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Ndg. Ngusa Samike ameupongeza uongozi wa hospitali ya wilaya ya Nachingwea kwa uboreshaji wa huduma za afya ambao umeenda sambamba na kuboresha miundombinu ya upatikanaji wa dawa katika duka la hospitali hiyo ikiwa ni mbadala wa utoaji wa Fomu 2C ambayo ilikua inampa mgonjwa anaetumia bima ya afya mbadala wa kwenda kupata dawa kwenye maduka ya dawa ya binafsi.
Akitoa mrejesho baada ya kukagua bohari ya dawa katika hospitali hiyo, Mfamasia wa Mkoa wa Lindi Ezekiel Bulyana amesema
“Nimekagua kwa kuanza na ujazaji wa nyaraka zote zinazotumika kupokea na kuingiza dawa nimeona zinajazwa vizuri kabisa kwa usahihi, lakini pia idadi ya dawa zilizopo ndani ya bohari ya dawa na duka la dawa la hospitali ni sawa na idadi zilizopo katika katika nyaraka husika, kitu kingine kizuri kilichopo hapa ni uwepo wa dawa ambazo kwa kipindi cha nyuma zilikua zinapatikana kwa kujaziwa Fomu 2C sasa baada ya kutolewa hawa hizo dawa wanazo hii inawapunguzia wagonjwa usumbufu wa kukosa dawa lakini pia hospitali inajiongezea kipato”
Aidha, kutokana na kukosekana na kipimo cha kaswende kwa wajawazito katika hospitali hiyo tangu mwezi Mei, kutokana na kukikosa MSD Katibu Tawala amesema
“kutokana na umuhimu na madhara ya kukosekana kwa kipimo hiko kwa mama mjamzito na mtoto aliyepo tumboni, tuangalie namna ya kukipata kipimo hiko kwa mshitiri, nawapongeza kwa uboreshaji wa duka la dawa na uwekaji wa kumbukumbu zilizo sahihi wa madawa, na nasisitiza ukusanyaji wa mapato na matumizi ya 50% ya mapato zitumike kama maelekezo yalivyotolewa, lakini pia maabara ya hospitali inahuduma ya vipimo vichache kuliko vile vinavyohitajika, hapa tunapaswa kuwa na vipimo kuanzia 80 hivyo vipimo viongezwe”
Pia, amewataka watumishi wa huduma ya kliniki na matunzo (CTC) kuhakikisha uwepo wa mipira ya kijikinga yaani kondomu katika maeneo ya faragha kama maeneo ya vyoo vya hospitali, maeneo ya kumbi za starehena sehemu za mikusanyiko ya watu kama sokoni na stendi za mabasi ili kuwapa urahisi watu kuzichukua kwa ajiri ya matumizi yao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.