Mhe. Zainab Telack Mkuu wa Mkoa wa Lindi ametoa maelekezo kwa viongozi wa Mkoa na wilaya kuhakikisha wananchi wanalima mazao ya chakula kwani wananchi wengi wanatumia fedha zao kidogo wanazozipata kutokana na mauzo ya mazao ya biashara (Korosho, Mbaazi na ufuta) kununua chakula badala ya kufanya shughuli za kimaendeleo na hata kushindwa kupeleka chakula shuleni kwaajili ya watoto wao .
Maelekezo hayo ameyatoa katika kikao cha kamati ya lishe mkoa Kilichowakutanisha wakuu wa wilaya wa Halmashauri zote, Wenyeviti za Halmshauri zote, wakurugenzi, makatibu Tawala, waatalamu wa afya kutoka Halmashauri na Mkoani na kujadili namna utekelezaji wa afua ya lishe inafanyika Mkoani Lindi .
Katika taarifa hiyo imebaini kuwa baadhi ya watoto wanazaliwa wakiwa na kilo pungugu na kusuasua kwa upatikanaji wa chakula kwa baadhi ya shule kunakosababishwa na usimamizi duni wa viongozi na walimu .
Kuyokana na hali hiyo Mhe Zainab amewataka maafisa elimu kuhakikisha shule zote zinalima mazao ya chakula na kuwataka wakuu wa wilaya kuona namna ya kutoa hamasa kwa wananchi ya kulima mazao hayo ili kupata chakula cha ziada na hatimaye kuondokana na changamoto ya upungufu wa chakula katika kaya .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.