Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Ufugaji Viumbemaji, Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Hamisi Nikuli Akizungumza mbele ya Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania, BOT kanda ya kusini Ndg. Nassor Omary katika banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya nanenane yanayoendelea kanda ya kusini amesema serikali imepanga kuwasaidia wakulima wa mwani kwa kuwapatia dhana za uzalishaji zao hilo. Dkt. Nikuli ameyaeleza hayo alhamisi ya tarehe 04 Agosti 2022 baada ya Mkurugenzi wa BOT kutembelea banda la Wizara hiyo.
Dkt. Nikuli amesema kuwa kwa sasa uzalishaji wa zao la mwani ni mdogo ukilinganisha namahitaji ya soko la kimataifa ambapo takribani tani 200,000 zinahitajika nje ya nchi kwa wiki. Lakini uzalishaji wake ni tani elfu 4 tu. Hivyo kwa kuanzia serikali imepanga kuwapatia dhana za kilimo hicho ili kusaidia kuongeza uzalishaji wa zao hilo na kufikia lengo lililowekwa la tani 15,000.
“ Sasa hiviuzalishaji wa mwani hauzidi tani elfu 4 kwa mwaka kwa Tanzania bara……..Zanzibar wanaenda mpaka tani elfu 11, mwaka uliopita walizalisha tani elfu 12……...Mwaka huu tumepanga kuzalisha tani 15,000 kwa kuanza lakini kitu ambacho walikuwa wanakwama ni uhaba wa pembejeo………mwaka huu tumejipanga kuwapelekea kamba, lakini pia tumepanga kuwapelekea taitai……….Tani elfu 15 kwa wakulima elfu 11, kwa tafiti zilizofanyika kwa kanda ya pwani kila mkulima akipata Kamba 200 za urefu mita 15, mita 20 anaweza kuvuna tani 1 mpaka tani 5 kwa mvuno mmoja na anavuta kila baada ya siku 45.” Amesema Dkt. Nikuli.
Aidha, Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania kanda ya kusini Ndg. Nassor Omary ameitaka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuimarisha mikakati ya masoko ya mwani hasa kutengeneza mfumo wa masoko ya mitandaoni ambao utarahisisha utangazaji wa mwanina bidhaa zake kwenye masoko ya ndani nan je ya nchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.