Hayo yamebainika jana jumatatu tarehe 01 Mei 2023 katika sherehe za wafanyakazi (Mei Mosi) Duniani ambazo kwa Mkoa wa Lindi zimeadhimishwa Wilayani Kilwa kwenye kiwanja cha Mkapa Garden ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack.
Hata hivyo Mhe. Telack hakuweza kushiriki katika Sherehe hizi za mkoa baada ya kupata mwaliko wa kushiriki maadhimisho yaliyofanyika kitaifa Mkoani Morogoro.
Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Lindi , Mhe. Christopher Ngubiagai ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, amesema kuwa ushirikiano wa wafanyakazi ndio msingi wa maendeleo yaliyofikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema kuwa Mkoa wa Lindi Kwa mwaka wa fedha 2022/23 umeletewa fedha za miradi kutoka serikalini kiasi cha Tsh. Bil. 318 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo mbalimbali katika sekta za afya, elimu, maji, barabara. Fedha hizi za miradi na maendeleo zimeleta tija na mafanikio makubwa kupitia Usimamizi na ushirikiano wa wafanyakazi.
Mhe. Mkuu wa Mkoa ameongeza kuwa pamoja na mafanikio yaliyopatikana, Serikali imeendelea kushughulikia changamoto mbalimbali za wafanyakazi wa Mkoa wa Lindi ambapo tayari imeajiri jumla ya wafanyakazi wapya 980, jumla ya wafanyakazi 1508 wameoandishwa madaraja na jumla ya wafanyakazi 169 wamebadilishiwa Kada.
Pia Serikali imeendelea kuboresha mifumo ya michango ya wafanyakazi ambapo kwa sasa michango inalipwa moja kwa moja kwenye mifumo ya jamii kupitia mifumo ya kisasa, Serikali inaendelea kufanyia kazi changamoto ya watumishi wanaolipwa na Serikali za Mitaa kupitia mapato ya ndani.Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa waajiri wote kuzingatia taratibu, Sheria, Kanuni na miongozo ya Serikali kuhakikisha wameandaa taarifa za mafao yao pamoja na kulipa stahiki za wastaafu kwa wakati ikiwemo gharama za kuwasafirisha nyumbani kwao.
Aidha, amewataka wafanyakazi kutumia vizuri masaa ya kazi na raslimali zilizopo katika kuleta tija na ufanisi. Ameongeza kuwa Taifa haliwezi kufikia maendeleo yaliyokusudiwa kwa kutangukiza tamaa na ubinafsi ikiwemo kutoa huduma kwa ubaguzi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.