Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Selemani Jafo (Mb) ametoa rai kwa Wananchi wa Wilaya ya Nachingwea kushirikiana katika kusimamia utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyopo Wilayani humo kwa ufanisi na tija na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa umma ili kutimiza malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita katika katika kutoa huduma bora za kijamii kwa Wananchi.
Aidha, aliwahakikishia Wananchi wa Wilaya hiyo kuwa Serikali ya Awamu ya Sita itaendele kutatua changamoto mbalimbali walizonazo na amewashauri kulinda, kutunza na kutumia vyema majengo na vifaa mbalimbali vilivyoweka kupitia Miradi hiyo ya Maendeleo pamoja na kuongeza kasi ya kutafuta hati ya ardhi kwa baadhi ya miradi ili kuhakikisha wanaendelea kupata huduma bora za afya, elimu, maji na mingineyo.
Waziri Jafo, ameyasema hayo Septemba 19, 2024 alipokagua, kuweka Jiwe la Msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuongea na kusikiliza kero za Wananchi wakati wa Ziara Maalum katika Wilaya ya Nachingwea Mkoa wa Lindi yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ikiongozwa na Kauli Mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone" iliyoanza tarehe 17 - 21/09/2024 Mkoani humo.
Aidha, amesema kuwa ameridhishwa na utekelezaji wa Miradi hiyo ya Maendeleo na kubainisha kuwa fedha zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita kwa ajili ujenzi wa shule na vituo vya afya imetumika vyema ambapo alikagua na kuweka Jiwe la Msingi katika Kituo cha Afya Lionja, Kituo cha Afya cha Kassim Majaliwa, Jengo la Kufulia, ICU, OPD, Maabara na Kichomea taka katika Hospitali ya Wilaya, ujenzi wa Bweni la Wanafunzi wenye uhitaji maalum Shule ya Msingi Chiwindi, Shule ya Msingi Nangunde pamoja na Mradi wa Maji wa Naipanga.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe. Mohammed Moyo ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani humo na kuahidi kuwa Wilaya yake itasimamia itekelezaji wa maagizo yote yaliyotolewa ilinkuhakikisha Miradi yote ya Maendeleo Wilayani humo inakamilika kwa wakati na kuanza kitoa huduma kwa wananchi katika muda uliopangwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.