Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndg. Abdalla Shaib Kaim Leo Ijumaa ametoa maagizo hayo katika Wilaya ya Kilwa muda mchache baada ya Mwenge wa Uhuru kufika Wilayani hapo.
Akizungumza na wananchi kwenye mradi wa ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha mirumba, Kata ya Kiranjeranje Wilaya ya Kilwa baada ya Mwenge wa Uhuru kufanya ukaguzi wa mradi huo, Ndg. Kaim ametoa maagizo kwa viongozi wote wa Wilaya kusimamia kwa ukamilifu ujenzi wa mradi huo ili urahisishe upatikanaji wa huduma za afya kwa kijiji cha mirumba na vijiji jirani.
Ndg. Kaim amesisitiza kuwa wananchi wanasubiri kunufaika na adhima ya Mhe. Rais ya kuimarisha miundombinu pamoja na kutoa huduma bora kwa jamii.
Ndg. Kaim amewapongeza wananchi wa kijiji cha mirumba kwa kuonesha uzalendo wa hali ya juu kwa kujitoa na kushirikiana kuanzisha ujenzi wa Zahanati yao.
Hivyo, Ndg. Kaim ametoa wito kwa wananchi wote kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuleta maendeleo kwa kujitoa na kujisimamia.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Christopher Ngubiagai amesema kuwa ujenzi wa mradi wa Zahanati ya kijiji cha mirumba ulianzishwa na wananchi wenyewe ili kuondokana na changamoto ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya.
Hivyo baada ya kuanzisha ujenzi huo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa fedha taktibani milioni 50 ili kukamilisha ujenzi wa Zahanati hiyo.
Mhe. Ngubiagai ameongeza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekwisha tenga kiasi cha fedha takribani milioni 200 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba vitakavyotumika baada ya ujenzi wa Zahanati hiyo kumalizika.
Aidha, Mbunge wa Jimbo la Kilwa kusini, Mhe. Ally Kassinge amemshukuru Rais kwa kusikia Kilio cha wananchi wa kijiji cha mirumba na kuchukua hatua za dhati katika kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa kijiji hicho na vijiji jirani.
Mhe. Kassinge ameiomba Serikali kujiandaa kupeleka wataalam watakao hudumu katika Zahanati hiyo pamoja na mahitaji yote ikiwemo vifaa vya matibabu pamoja na dawa.
Mhe. Kassinge amewaahidi wananchi wa Jimbo lake kuwa ataendelea kutumia nafasi ya uwakikishi wao bungeni Kuomba fedha zaidi Kwa ajili ya maendeleo ya kijiji cha mirumba na Kilwa kusini Kwa ujumla.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.