Hayo yamesemwa jana tarehe 22 Juni 2023 na Mhe. Shaibu Ndemanga, Mkuu wa Wilaya ya Lindi akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Lindi katika kikao cha wadau wa Wakala ya Ufundi na Umeme, TEMESA kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Mhe. Ndemanga amezitaka mamlaka zote za Serikali kuendelea kutumia huduma za Wakala wa Ufundi na Umeme, TEMESA kwa kuwa taasisi hiyo imeboreshwa kwa kiasi kikubwa.
Mhe. Telack amewaeleza wakuu wa taasisi waliohudhuria kikao hicho kuwa TEMESA ya sasa ina vifaa vizuri na huduma ya Karakana inayotembea (mobile workshop) ambayo inatolewa kupitia gari maalum lililotolewa na Serikali kwa ajili ya kuhudumia mikoa ya kanda ya Kusini, Lindi na Mtwara.
Aidha, Mhe. Ndemanga ameitaka taasisi hiyo pamoja na kufanya maboresho kwenye eneo la vifaa izingatie pia maboresho katika utendaji hasa eneo la utaalam wa utengenezaji wa vyombo vya usafiri.
Mhe. Ndemanga ameongeza kuwa maboresho hayo yaendane na ubora wa huduma inayotolewa jambo ambalo litaimarisha na kuongeza imani kwa wateja.
Akizungumza kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa TEMESA Ndg. Razaro Kilahala amesema kuwa kwa sasa changamoto zilizokuwa zikirudisha nyuma jitihada za TEMESA zimefanyiwa kazi na kurekebishwa ambapo tayari yamefanyika maboresho kwenye maeneo yote ikiwemo mfumo wa ununuzi wa vipuli utakaosaidia kuepuka na kudhibiti matumizi ya vipuli feki.
Awali akieleza mbele ya mgeni rasmi namna ya utoaji wa huduma kupitia Karakana inayotembea ( mobile workshop), Fundi Mkuu wa huduma hiyo kwa kanda ya pwani na Kusini Ndg. Mustapha Abdul amesema kuwa huduma ya mobile workshop inapatikana kwa masaa 24 na inamfuata mteja popote alipo.
Ndugu Mustapha ameongeza kuwa huduma hii inampungizia mteja gharama nyingi ikiwemo mafuta ya kuitoa gari ofisini na kuipeleka kwenye huduma ya matengenezo.
Kupitia maboresho yaliyofanywa na Wakala wa Ufundi na Umeme, TEMESA kunaondoa mashaka ya wateja kuhusiana na huduma zinazotolewa na taasisi hiyo ambapo itakuwa kivutio kikubwa si tu kwa taasisi za Serikali lakini pia hata kwa wateja binafsi wa vyombo vya usafiri
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.