Taasisi ya kupambana na rushwa, PCCB Wilaya ya Kilwa imeagizwa kufanya uchunguzi wa fedha na maendeleo yasioridhisha ya ujenzi wa bweni la watoto wenye mahitaji maalum unaendelea katika Shule ya Msingi Mtanga iliyopo Kilwa Masoko, Wilayani Kilwa kwa fedha za Maadhisho ya Uhuru wa Tanzania bara ya mwaka 2022.
Maagizo hayo yametolewa Leo tarehe 14 Aprili 2023 na kiongozi wa Mwenge wa Uhuru ndg. Abdalla Shaib Kaim baada ya Mwenge wa Uhuru kutembelea na kukagua mradi huo ulioanza kujengwa tarehe 05 Februari 2023.
Akiweka jiwe la msingi kwenye mradi huo, ndg. Kaim amesema kuwa kutokana na ukaguzi uliofanyika zimebainika changamoto zinazohusu mradi ikiwemo kwenye ghala la kuhifadhia bidhaa za ujenzi wa mradi.
Ndg. Kaim amekili kutokuwa na mashaka juu ya ubora wa mradi, kuwa ni wa kuridhisha lakini changamoto kubwa ni mradi kuchelewa kumalizika kwa wakati. Ameongeza kuwa mradi umechelewa kumalizika lakini wataalam hawana majibu yanayotosheleza ni kwa nini mradi haumaliziki.
Aidha, Ndg. Kaim ameongeza kuwa watoto wenye mahitaji maalum wanahitaji kuyatumia mabweni mapya kwa mahitaji yao ambayo yatawapa fursa ya kupata elimu bora.
Awali akisoma taarifa ya mradi huo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mtanga Omary Mohamed amesema kuwa fedha za mradi wa bweni zilipatikana baada ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kufanya maamuzi ya kubadilisha matumizi ya fedha za Maadhimisho ya Sherehe za Uhuru yaliyotakiwa kufanyika mwaka 2022.
Baada ya mabadiliko hayo, Shule ya Msingi Mtanga ilipatiwa jumla ya Tsh. Milioni 110 mwezi Disemba 2022 kwa ajili ya ujenzi wa bweni lenye uwezo wa kuchukua jumla ya watoto 80 wenye mahitaji maalum likiwa na vyumba 20, matundu ya vyoo 5, mabafu 5.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Christopher Ngubiagai amemshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha ujenzi wa miundombinu rafiki itakayowasaidia watoto wenye mahitaji maalum kupata fursa ya elimu katika mazingira rafiki.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.