.
Katibu Tawala Msaidizi ndugu Natalis Linuma amewapokea na kuwakaribisha maafisa kutoka kituo cha uwekezaji Tanzania ( TIC ) kujionea fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana Mkoani Lindi na namna ambavyo wananchi wa ndani ya Mkoa na nje ya Mkoa walivyowekeza .
Hii ni mwendelezo wa kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha uwekezaji wa ndani ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na dhamira ya dhati ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuhakikisha wananchi wanawekeza katika maeneo mbalimbali ndani ya nchi ya Tanzania. .
Kampeni hii inakwenda sambamba na utoaji wa elimu ya uwekezaji kwa makundi mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara, wawekezaji wa ndani pamoja na waandishi wa habari .
#karibulindi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.