Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Shaib Ndemanga akiwa ni mgeni rasmi ametoa maelekezo hayo kwa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Lindi, TRA kwenye maadhimisho ya wiki ya Mlipa Kodi iliyoadhimishwa Jumamosi ya tarehe 07 Oktoba 2023 katika viwanja vya fukwe pembezoni mwa Hoteli ya Sea View.
Mhe. Ndemanga akizungumza na walipa kodi pamoja wa wageni waalikwa walioshiriki maadhimisho hayo, amesema kuwa kwa sasa Mkoa wa Lindi unafunguka kwa Kasi kubwa hivyo Mamlaka ya Mapato iyatambue maeneo yote yatakayoongeza mapato ya Serikali hasa kupitia sekta ya madini ambayo uwekezaji wake unakua kwa kasi.
Mhe. Ndemanga pia ameitaka Mamlaka hiyo ya Mapato ijipange vizuri kukusanya Kodi kupitia msimu wa manunuzi wa zao la korosho ili kuhakikisha wadau wote wanaotakiwa kulipa kodi wanawajibika inavyotakiwa.
Aidha, Meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Lindi Bi. Matilda Kunenge amesema kuwa Mamlaka ya Mapato imekuwa ikifanya vizuri kutokana na ushirikiano mzuri uliopo Kati ya Mamlaka hiyo na walipa Kodi wa Mkoa wa Lindi.
Pamoja na ushirikiano huo, Bi. Matilda Amewasihi wadau kujitokeza na kuwa wazi kwa Mamlaka hiyo ili kila mmoja ashiriki katika kuchangia maendeleo yanayoonekana Mkoa wa Lindi ikiwemo barabara zenye taa nzuri, hospitali, huduma za maji na kadhalika.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa wafanyabiashara Ndg. Ahmad Mikapa amesema kwa sasa ushirikiano Kati ya Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Lindi na walipa Kodi hasa wafanyabiashara umeimalika kwa kiwango cha juu ukilinganisha na miaka kadhaa iliyopita.
Ndg. Mikapa ameongeza kuwa kwa sasa changamoto mbalimbali zinazoibuka zimekuwa zikitatuliwa kwa ushirikiano wa pamoja Kati ya Mamlaka ya Mapato na wafanyabiashara Jambo ambalo limechangia maendeleo ndani ya mkoa kwa kiasi kikubwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.