#Picha za matukio mbalimbali za hafla ya kumuaga aliyekuwa katibu Tawala Msaidizi uchumi na uzalishaji Ndugu Majid Myao iliyofanyika katika ukumbi mkubwa wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi Februari 28, 2028 .
Akimkaribisha mgeni rasmi wa hafla hiyo , Katibu Tawala Msaidizi eneo la uchumi na uzalishaji Ndugu Mwinjuma Mkungu ametoa sifa za kiungwana za Ndugu Majid Myao mstaafu akiwa katika nafasi hiyo kabla ya kustaafu .
Mkungu, amesema kuwa ofisi ya katibu Tawala eneo la uchumi na uzalishaji imeandaa hafla hiyo kwa lengo la kuonesha uungwana ule ule ambao kiongozi mstaafu ameuonesha kwa watumishi wenzake na namna ambavyo alikuwa anatoa huduma kwa wananchi.
Katika kuonesha upendo huo , licha ya hafla ambayo wameandaa, wamekabidhi zawadi mbalimbali ikiwemo jiko la gesi.
Kwa upande wake katibu Tawala Msaidizi eneo la utawala Ndugu Nathalis Linuma kwaniaba ya katibu Tawala Mkoa wa Lindi amempongeza na kumkabidhi zawadi ya ofisi, ikiwa sehemu ya kutambua mchango wake katika utumishi wa umma .
Aidha, ametumia fursa hiyo kuwasihii watumishi wengine kujifunza weledi wa mstaafu mzee Majid Myao katika utumishi wa umma.
Akishukuru kwa hafla na zawadi hizo Ndugu Majid Myao amesema kilichofanyika ni upendo ambayo ametendewa hakutegemea mkusanyiko huo na zawadi ambazo amezipata .
Ametumia fursa hiyo kumshukuru Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainabu Telack Zuwena, katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary pamoja na watumishi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ushirikiano ambao ameuonesha kwa kipindi chote cha utumishi wa umma.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.