• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

UJENZI WA MADARAJA YA DHARURA HAUTAATHIRI MIPANGO YA KUDUMU : WAZIRI ULEGA

Posted on: April 8th, 2025

Serikali imefafanua kwamba kazi ya ujenzi wa madaraja matano kwenye barabara kuu ya Dar es Salaam - Lindi zilikuwa zinaendelea na haitaathiriwa na juhudi za sasa za kukarabati maeneo yaliyoharibiwa na mafuriko ya mvua katika siku za karibuni.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa leo na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, katika eneo la Somanga na Matandu mkoani Lindi ambapo anasimamia ukarabati wa dharura wa barabara iliyoharibiwa na mvua.


Ulega alitumia fursa hiyo kutangaza pia kwamba serikali tayari imetenga fedha kwa ajili qpya ujenzi wa madaraja ya kudumu na ni kazi endelevu hadi itakapokamilika.


“Tutambue kuwa ujenzi wa madaraja sio suala la wakati mmoja ni la hatua kwa hatua. Niwatoe hofu Watanzania kwamba toka ilipotokea dharura mwaka jana ya kukatika maeneo hayo Serikali imechukua hatua madhubuti na kila mahali yupo Mkandarasi anafanya wajibu wake”, amesisitiza Ulega.

Aidha, Ulega amewahakikishia Watanzania kuwa huduma za usafiri na usafirishaji kwa mikoa ya kusini zimerejea  tangu alfajiri na zinaendelea kuimarika ambapo magari madogo, mabasi ya abiria na magari makubwa ya mizigo  yanaendelea kupita katika eneo la Somanga na Matandu ili wananchi waweze kuendelea na safari.


Hatahivyo, Ulega ametoa wito kwa wananchi waliosimama  kituo cha Mabasi yaendayo Mikoa ya Kusini cha Mbagala kutokana na hofu ya kushindwa kuvuka katika eneo la Somanga - Mtama kuendelea na safari kwani eneo hilo sasa ni salama  na linapitika.

Ulega amewashukuru wananchi wote waliokumbwa na changamoto hiyo kwa uvumilivu na subira pamoja na kuwapongeza Wakandarasi  na Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na TANROADS kwa kushiriki zoezi hilo usiku na mchana ili kuhakikisha mawasiliano yanarajea.


@wizara_ya_ujenzi

@zainabutelacky

@ortamisemi

@maelezonews

@msemajimkuuwaserikali

@owm_tz

@kilwa_dc

Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • JAMII NA WAZAZI WATAKIA KURUDI KUBEBA JUKUMU LA MALEZI KWA WATOTO

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA WA LINDI AONGOZA KIKAO CHA LISHE NGAZI YA MKOA

    May 03, 2025
  • MHE. TELACK AZINDUA MPANGO MKAKATI WA ELIMU MKOA WA LINDI KWA MWAKA 2025

    May 02, 2025
  • RC TELACK AKABIDHI TUZO ZA ELIMU KWA WALIMU,WANAFUNZI NA HALMASHAURI ZILIZOFANYA VIZURI MKOANI LINDI.

    May 02, 2025
  • tazama zote

Video

CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA CHAMA CHAO MAPEMA ILI KUWAPA UTULIVU WANACHAMA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO ILI WANACHAMA WAPATE UTULIVU

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.