Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zaina Telack @zainabutelacky ameridhishwa na hatua ya ujenzi wa Tawi la Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kinachojengwa Ngongo- Ruangwa Lindi ambapo upande wa Ngongo ujenzi umefikia 45% na Ruangwa umefikia 36% .
Awali akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa mradi huo Mhandisi wa mradi upande wa Mkandarasi Ndugu Ramadhan Ihimbilo amesema kuwa ujenzi wa Tawi la Chuo kikuu cha Dar Es Salaam kinachojengwa Ngongo –Ruangwa Lindi hadi sasa umefikia 45% kwa upande wa Ngongo na upande wa Ruangwa umefikia 36%.
Mhe. Telack, akimsisitiza mkandarasi kuendelea kuzingatia kasi na ubora wa ujenzi amesema kuwa mradi huo ni maono ya Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wananchi wake wa mkoa wa Lindi ambao asilimia kubwa ya uchumi wao unategema kilimo na ndiyo maana hivi karibuni amezindua benki ya ushirika kwa ajaili ya wakulima.
Aidha Mradi huu kwa awamu ya kwanza unajumuisha ujenzi wa majengo Sita ya chuo kwa Ngongo na Majengo Matatu ya Chuo kwa Likunja na ujenzi huo unajumuisha miundombinu saidizi ikiwepo Barabara, maji na umeme.Mkataba wa utekelezaji wa mradi awamu ya kwanza ni wa miezi 18 na unatekelezwa na kampuni ya Shandong Hi- Speed Dejian Group Co. Ltd na mradi ulianza kutekelezwa tarehe 21/03/2024 naunatarajiwa kukamilika 19/9/2025. Mpangilio wa ujenzi wa Chuo - Tawi la Ngongo, Manispaa ya Lindi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mh. Victoria Mwanziva @victoria.mwanziva amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwa ziara hiyo na kuahidi kutekeleza maelekezo yote ambayo ameyatoa ili kulete ufanisi wa mradi huo.
Kutokana na hatua hiyo , Mhandisi Ramadhani Mbonje amesema ujenzi unatarajiwa kukamilika kwa wakati .
Hadi sasa mradi huu umetumia Tsh Bil 4.1 katimya Bilioni 13..
@maelezonews
@ortamisemi
@owm_tz
@msemajimkuuwaserikali
@udsmofficial
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.