Maafisa uandikishaji mkoa wa Lindi wataakiwa kusimamia zoezi la uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura.
Hayo yamesemwa na Kamishina Tume ya Taifa Uchaguzi, Jaji (Mst.) Thomas Mihayo wakati hakifungua mafunzo kwa wandikishaji yaliyo wausisha Afisa Mwandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi Ngazi ya Jimbo, Afisa Uchaguzi wa Halmashauri na Maafisa Tehama.
Jaji Mihayo amesema kuwa mafunzo hayo yanatolewa ili kuwawezesha washiriki kupata uelewa wa jukumu wanalokwenda kulitekeleza na ili na wao waweze kwenda kuwafundisha waliopo katika ngazi ya kata na tarafa.
Washiriki wametakiwa kuelewa maelekezo wanayopewa na kuhakikisha wanakuwa makini katika kusimamia utekelezaji wa zoezi hilo.
“Zoezi hili la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ni la muhimu sana kwani ndio mchakato wa uchaguzi mkuu unaanza. Hivyo wataalam wote watakaohusika kusimami zoezi hilo wanapaswa kuwa makini na kulichukulia zoezi hilo kwa uzito unaostahili”, alisema Jaji Mihayo.
Pia alieleza kuwa uboreshaji huu wa taarifa katika daftari la kudumu la wapiga kura ni haki ya kila mwananchi ambaye ametimiza umri wa miaka 18 pamoja na vigezo vingine. Hata hivyo endapo mwananchi yeyote ambaye atakutana na kikwazo chochote wakati zoezi hili la uandikishaji likiendele anatakiwa kutoa taarifa kwa uongozi ili suala lake lishughulikiwe kwa wakati.
Kwa upande wa mawakala wa vyama vya siasa, Jaji Mihayo amesema kuwa wanayohaki ya kwenda kuona namna zoezi la uboreshaji daftarri linavyokwenda na kutoa maoni/malalamiko pale wanapoona mambo hayapo sawa lakini sio kuingilia mchakato wa zoezi lenyewe.
Naye Afisa Uandikishaji halmashauri ya Nachingwea, Hassan A. Rugwa amesema wamejipanga kuhakikisha zoezi hilo linaendeshwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu kama zilivyowekwa, na kwamba watahakikisha wale wote watakaojitokeza na wenye vigezo vinavyostahili wanajiandikisha/kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la wapiga kura. Hivyo wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi na kutumia fursa hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.