Kero ya uvamizi wa wanyamapori katika maeneo ya makazi na shughuli mbalimbali za binadamu kama kilimo bado ni changamoto kwa wakazi wa tarafa ya Kibutuka iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
Kero hiyo imetolewa kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Mhe. Ngusa Dismas Samike, alipokuwa anafanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri ya Liwale tarehe 17/08/2022.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi Diwani wa kata ya Kibutuka Bwana. Faraja Said Nyihira amesema “Kero ya uvamizi wa wanyamapori hususani Tembo limekua tatizo sugu katika eneo hili, Tembo wamekuwa wakiingia katika mashamba na kufanya uharibifu wa mazao ya chakula na wakati mwingine wamekuwa wakivamia hadi maeneo ya makazi ya wananchi na kwenye mashule hali inayopelekea wanafunzi wetu kutokusoma kwa utulivu wakihofia kuvamiwa wakati wowote na tembo hao”
Aidha, Katibu Tawala ametoa ufafanuzi kuwa tayari serikali ilishaunda timu ya uchunguzi wa madhara ya uvamizi wa wanyamapori katika maeneo ya shughuli za kibinadamu ambapo baada ya uchunguzi huo mikakati mbalimbali imewekwa ili kuzuia tatizo hilo.
“Kutakua na ujenzi wa kituokazi ili kuhakikisha uwepo wa wafanyakazi wa TAWA kwa wakati wote, na kituo hiko kitakua kinafanya kazi muda wote na kitakua cha kudumu ili wafanyakazi hao basi watusaidie katika udhibiti uvamizi wa wanyamapori hawa, lakini pia tutaongeza na idadi ya wafanyakazi wa TAWA hasa katika maeneo ambayo uvamizi wake ni mkubwa na hii itaenda sambamba na kudhibiti uvamizi wa mifugo inayoletwa na wenzetu wafugaji hivyo uongozi wa wilaya muafikiane ni njia gani mbadala tunaweza kuitumia katika kutatua changamoto hii” Mhe. Ngusa Samike.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.