Kuelekea kilele cha miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Mkuu wa mkoa wa Lindi Mh. Bi. Zainab Telack amezindua nyumba 3 za watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa zilizogharimu kiasi cha shilingi milioni 255,002,585 ambapo vifaa vya ujenzi vimegharimu shilingi milioni 204,772,585 na shilingi milioni 50,230,000 zimetumika kwa gharama za ufundi.
Katika uzinduzi huo, Katibu Tawala Msaidizi, Utawala na Rasilimali watu, Dkt. Bora Haule amesema kuwa ujenzi wa nyumba hizo ulioanza Julai 4, 2021 kwa mkataba wa miezi mitatu na kukamilika kwa asilimia 100, una lengo la kujenga nyumba 13 za wakuu wa sehemu na vitengo, ambapo shilingi milioni 360 zimetengwa kwa ajili ya awamu ya pili ya ujenzi wa nyumba nne maeneo ya mitwero, Lindi Manispaa.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Bi. Zainab Telack amewataka watumishi waliokabidhiwa nyumba hizo kuzitunza na kuhakikisha zinakua katika hali ya usafi muda wote ‘ ‘Nyumba hizi zitunzeni vizuri ili hata baada ya kumaliza majukumu yenu wengine wakabidhiwe zikiwa nzuri na safi, uharibifu wowote ule kama kuchorwa kwenye kuta mutawajibika kurekebisha. Lkini pia nyumba zinazotarajiwa kuendelea kujengwa zitakua nzuri zaidi ya hizi’’
Akitoa neno la shukrani, Katibu Tawala Msaidizi, Uchumi na Uzalishaji, Ndg.Majid A. Myao amesema ‘‘ nyumba hizi zitatusaidia kutekeleza na kuwahi majukumu yetu hivyo tunashukuru kwa uthamani huu wa kupatiwa nyumba hizi, tutajitahidi kuzitunza vizuri na kuzikabidhi zikiwa katika hali nzuri. Aidha, niishukuru kamati iliyosimamia ujenzi wa nyumba hizi kwa uratibu mzuri wa mradi huu hadi hatua hii iliyofikiwa leo. ’’
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.