Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amepongeza utekelezaji wa usambazaji huduma ya Nishati ya Umeme vijiji chini ya wakala wa usambazaji huduma hiyo REA kwa kufanikisha utekelezaji kwa asilimia Miamoja kwani vijiji vyote 523 vya Mkoa wa Lindi vimefikiwa na huduma ya umeme.
Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa usambazaji umeme vijijini Mkoa wa Lindi , Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali (mstaafu), Jacob Kingu amesema kuwa REA imefanikiwa kufikisha huduma ya umeme katika Vijiji vyote 523 .
“Leo ni siku ya furaha sana kwetu na kwa Wananchi wa Mkoa wa Lindi. Mkoa wa Lindi una jumla ya Vijiji 523 na vijiji vyote sasa tumeshavifikishia huduma ya umeme. Hatuna deni na Wananchi wa vijiji vya Mkoa huu,” amesema Mwenyekiti Kingu.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo Mei 7, 2025 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali (mstaafu), Jacob Kingu amesema kuwa REA sasa inaendelea na kupeleka umeme katika Vitongoji.
Ameongeza kuwa, Mkoa huo una jumla ya vitongoji 2406 na vitongoji 1481 tayari vimeshafikishiwa umeme huku vitongoji 442 wakandarasi wako wanaendelea na kazi.
Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya Mwenyekiti wa REB, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab Telack amempongeza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kutoa fedha zilizofanikisha mradi huo kukamilika kabla ya muda uliopangwa.
“Mhe. Rais anaendelea kuonesha nia yake ya kutamani kuwaletea maendeleo Watanzania. Tunapenda kumpongeza sana Mhe. Rais, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na Watendaji wote wa Serikali waliowezesha ndoto hii kutimia,” amesema Mhe. Telack.
Ameongeza kuwa, uwepo wa umeme vijijini licha ya kuboresha huduma za kijamii katika vijiji, utasaidia kuinua uchumi wa wananchi kwa kufanya shughuli mbalimbali zitakazowaongezea kipato.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Umeme Vijijini kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu amewaomba viongozi kuendelea kuwahamasisha wananchi kulinda miundombinu ya umeme kwa kuwa serikali imeto
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.