Naibu waziri Angelina Mabula amewataka viongozi wa mkoa wa Lindi kuchukua hatua kwa wamiliki wa mashamba yote yaliyotelekezwa na yasiyoendelezwa.
Mhe. Mabula ameyasema hayo katika kikao chake alichofanya katika ofisi ya mkuu wa mkoa, kikao amabacho kiliwahusisha viongozi katika sekretarieti ya mkoa, taasisi zilizo chini ya wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, pamoja na wataalam wa ardhi kutoka manispaa ya Lindi.
Naibu waziri mabula amesema mkoa unajumla ya mashamba makubwa 136 kati ya hayo mashamba 60 yameendelezwa, mashamba 56 yametelekezwa huku mengine yakiwa hayajaendelezwa.
Hivyo ameuagiza uongozi wa mkoa kuhakikisha wanazisimamia halmashauri zichukue hatua kwa wamiliki wa mashamba hayo ikiwa ni pamoja na kuwaandikia ilani ya siku 14 ya kuwataka wayaendeleze mashamba hayo. Aidha pamoja na kuwapa ilani watapaswa pia kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kuwany’ang’anya endapo hakutakuwa na majibu au uendelezaji kutokana na ilani waliyowapatia.
Kuhusu mashamba ambayo yamefutwa umiliki wake na kurejeshwa serikalini, Mhe. Mabula amezitaka halmashauri kutokimbilia kupima viwanja badala yake wanatakiwa kuandaa mipango ya matumizi ya mashamba hayo ikiwa ni pamoja na kutafuta wawekezaji wengine ambao watakuwa tayari kuja kuwekeza kwa shughuli mbalimbali.
Vilevile uongozi wa mkoa umeagizwa kufanya tathmini katika mashamba yote makubwa ili kuona hali ya uvamizi katika mashamba hayo na kuona ni namna ya kufanya katika kuzuia uvamizi huo.
Hivyo basi amewataka viongozi wa halmashauri na manispaha ya Lindi kuongeza kasi ya upimaji wa maeneo na urasimishaji makazi, ikiwa ni pamoja na upimaji wa maeneo ya serikali ili yasivamiwe. Pia ameziagiza halmashauri kuwa na mkakati maalumu wa ukusanyaji maduhuri ili ziweze kufikisha malengo yariyo wekwa kwani kwa sasa hali ya ukusanyaji hipo chini. Hii ni pamoja na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa kisheria wamiriki wote wa viwanja na mashamba amabao wajaripa kodi za ardhi.
Waziri Mabula alisema licha kwamba kuna shida ya watumishi nchi mzima, tunatakiwa kuwa na watumishi 2900 katika idara ya ardhi nchi nzima lakini tunawatumishi 1500 na kupungukiwa na watumishi wanaopata 1400, hivyo aliwataka watumishi waliopo wafanye kazi kwa bidii katika taasisi na halmashauri walizopangiwa wakati serikali ikiendelea na jitihada zakuajiri watumishi wengine .
Aidha, amewasihi viongozi kuhakikish wanatembelea masijara za ardhi zilizopo katika maeneo yao kwani kuwepo na tatizo la utuzaji mbovu wa fairi, mafairi kukosa nyaraka za msingi na mafairi kutoonyesha mawasiliano kati ya afisa mmoja kwenda kwa mwingine pamoja na ucheleweshwaji wa utengezaji wa hati.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.