• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Menejimenti ya Serikali za Mtaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Kilwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Lindi
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Liwale
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Nachingwea
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
    • Ruangwa
      • Historia ya Wilaya
      • Uongozi wa Wilaya
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
    • Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Liwale
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Jarida
    • Fomu
    • Sheria
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

VIONGOZI WA MKOA WA LINDI WATAKIWA KUWA NA WELEDI KATIKA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA MPANGO JUMUISHA WA AFYA NGAZI YA JAMII

Posted on: June 10th, 2024

LINDI:  VIONGOZI WATAKIWA KUWA NA WELEDI KATIKA UTEKELEZAJI WA  MPANGO JUMUISHI WA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII.


Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Zainab Telack amewasihi viongozi wa wilaya na mkoa kuzingatia Weledi katika utekelezaji wa Mpango jumuishi wa wahudumu wa afya ngazi ya jamii kwa Mkao wa Lindi .


Mhe. Ndemanga ameyasema hayo leo Juni 10, 2024 katika utambulisho wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya ngazi ya jamii uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha uuguzi Lindi na kuhudhuriwa na viongozi wa Wilaya na Mkoa .


“Niwakumbushe mambo mawili ya msingi, moja tunapaswa kuwa na weledi katika utekelezaji wa mpango huu, kwani yapo mambo mengi ambayo yanaweza kuibuka wakati wa utekelezaji hasa katika zoezi la kuchagua watoa huduma ambao kimsingi wanachaguliwa na wanajamii wenyewe “ Mhe. Ndemanga.


Mhe. Ndemanga ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wataalam ngazi ya wilaya na mkoa juu ya umuhimu wa kutunza kumbukumbu vizuri, ambazo zinasaidia sana kuondoa sintofahamu wakati wa utekelezaji na baada ya utekelezaji wa kuwapata watoa huduma ngazi ya jamii na shughuli zingine muhimu za kiutendaji.


“ Bila shaka mnafahamu juu ya umuhimu wa kumbukumbu, hivyo katika zoezi hili tunapaswa kuzingatia kuweka kumbukumbu sawa kama ambavyo mazoezi mengine yalivyofanyika vizuri “


Kwa upande wake Bi. Orsolina Tolage  ambaye ni Afisa progamu wa mpango wa Huduma za Afya ngazi ya jamii kutoka Wizara ya Afya Idara ya Kinga, Sehemu ya Elimu ya Afya Kwa Umma ameeleza  malengo ya mpango huo pamoja na kuzuia magonjwa yasiyo ambukiza kama vile Malaria, Magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora pamoja na magonjwa yanayotokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.


Na Afisa Maendeleo ya Jamii idara ya Serikali za Mitaa Ofisi ya Rais –TAMISEMI Ndugu Jeremiah Mwambange akieleza muongozo wa utaratibu wa kuwapata wahudumu wa Afya ngazi ya jamii amesema kuwa, jamii ndiyo yenye jukumu la kumchagua mhudumu wa Afya ngazi ya jamii kadri watakavyoona anafaa kuwahudumia kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa .


Serikali imeweka utaratibu wa kuwapa mafunzo ya kuwajengea uwezo wahudumu tajwa kupitia vyuo vya Afya vya kati na hatimaye kuwawezesha kutekeleza majukumu ngazi ya jamii kwa kuwapa vitendea kazi na motisha.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALI0CHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021-MKOA WA LINDI March 29, 2021
  • Vitabu vya kalenda za utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari February 08, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA MKOA WA LINDI 2022 May 09, 2022
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI KWA MKOA WA LINDI (JOINING INSTRUCTIONS) December 16, 2020
  • tazama zote

Habari Mpya

  • JAMII NA WAZAZI WATAKIA KURUDI KUBEBA JUKUMU LA MALEZI KWA WATOTO

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA WA LINDI AONGOZA KIKAO CHA LISHE NGAZI YA MKOA

    May 03, 2025
  • MHE. TELACK AZINDUA MPANGO MKAKATI WA ELIMU MKOA WA LINDI KWA MWAKA 2025

    May 02, 2025
  • RC TELACK AKABIDHI TUZO ZA ELIMU KWA WALIMU,WANAFUNZI NA HALMASHAURI ZILIZOFANYA VIZURI MKOANI LINDI.

    May 02, 2025
  • tazama zote

Video

CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO YA CHAMA CHAO MAPEMA ILI KUWAPA UTULIVU WANACHAMA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Watumishi Portal
  • Kilwa District Council
  • Nachingwea Disctrict Council
  • Ruangwa District Council
  • Liwale District Council
  • Lindi Municipal
  • Lindi District Council

Kurasa mashuhuri

  • Public Procurement Reguratory Authority
  • Tamisemi
  • e-Government Agency
  • Watumishi Portal
  • Sekretarieti ya ajira
  • CWT WASHAURIWA KUMALIZA MIGOGORO ILI WANACHAMA WAPATE UTULIVU

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

    Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi

    Simu: 023-220-2098

    Rununu:

    Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.