Wadau wa masuala ya Kilimo hai wameomba serikali kutambua na kuthamini matumizi ya mbegu za asili hali itakayochochea ulaji wa vyakula vya asili visivyo na kemikali nchini.
Hiyo ni kutokana na Mbegu asili kuwa ndiyo msingi wa kilimo, huku uhakika na usalama wa mbegu hizo kwa wakulima wadogo hapa nchini ambao ndiyo wazalishaji wakuu wa chakula ukitajwa kuwa ni muhimu katika kuhakikisha kuna usalama wa chakula.
Wameomba hayo katika uzinduzi wa siku maalum ya mbegu za asili iliyofanyika tarehe 06 Agosti, 2022 wakati wa maadhimisho ya maonyesho ya nanenane kanda ya kusini yaliyohitimishwa tarehe 08 Agosti 2022 katika viwa nja vya Ngongo mkoani Lindi ambapo lengo kuu likiwa kuhamasisha wakulima na jamii kwa ujumla kutumia mbegu na vyakula vya asili.
Mtaalam kutoka SWISSAID Bwa. Daudi Ngosengwa na mdau wa SWISSAID Bwa. Abdallah Ramadhani wamesema kuwa kwa sasa wanahitaji watunga sera, kutunga sera ambazo zitawasaidia wakulima kuuza mbegu zao za asili kama ilivyo kwa mbegu zingine.
Wadau hao wameeleza kuwa, katika kuifikia ajenda ya 10/30 vyanzo vikuu viwili vya mbegu vinavyotegemewa na Wakulima katika kuendesha shughuli zao za kilimo ambavyo ni mfumo wa mbegu ulio rasmi wa kibiashara na mfumo usiokuwa rasmi ikisimamiwa na kuwezeshwa vizuri ina mchango mkubwa wa kufikia lengo la serikali la ajenda hiyo ambayo inataka ifikapo 2030 sekta ya kilimo ikue na kuchangia pato la taifa kwa 10%.
kwa upande wake mkurugenzi msaidizi wa idara ya mbegu kutoka wizara ya kilimo Beatus Malema ameeleza kwamba taifa halitakiwi kuziacha mbegu za asili zipotee kwani itakuwa ni hasara kwenye sekta ya kilimo kwa maana watafiti hawatakuwa na chanzo cha uhakika cha kupatia nasaba za mimea kwa ajili ya tafiti zao. Ameongeza kuwa mbegu za asili zinaongeza wigo mpana wa baoanuai na hatimaye uhakika wa upatikanaji wa viini lishe ambavyo ni muhimu katika kutokomeza matatizo ya utapia mlo.
kwa mujibu wa mkurugenzi wa SWISSAID Bi. Betty Malaki amesema kuwa siku ya maonyesho ya mbegu za asili huwakumbusha walaji baadhi ya vyakula ambavyo vilikuwa maarufu siku za nyuma lakini sasa havionekani kupendwa na walaji lakini pia vinajulisha mahusiano yaliyopo kati ya jamii na mila na desturi zao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.