Wakati wa Kata ya Lionja iliyopo Halmashauru ya Wilaya ya Nachingwea wapo mbioni kuondokana na changamoto ya uhitaji wa kituo cha afya katika kata yao.
Matumaini hayo mapya yameibuka baada ya Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Seleman Jafo kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa kituo cha afya Lionja ambacho kinatarajiwa kuhudumia jumla ya wakazi elfu 6519 waliopo katika kata hiyo na vijiji jirani kama Nditi, Ndamikango na Ngumichile.
Kituo hiko cha afya kinachotarajiwa kufunguliwa rasmi Disemba 30 mwaka huu na kuanzishwa huduma za awali , kinajumuisha majengo kama jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje yaani OPD, jengo la maabara, jengo la kufulia na kichomea taka.
Bahati Mteta, Elidia Medradi na Bwana. Christopher Nchumbo wakazi wa kata ya Lionja, wameeleza matumaini yao mara baada ya kufunguliwa rasmi kwa kituo hicho ambacho kitawapunguzia gharama za kusafiri umbali mrefu na kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.
Waziri Jafo yupo mkoani Lindi kwa ziara maalumu ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendelek ambayo serikali imeleta kwa wananchi chini ya kauli mbiu isemayo 'Rais Samia na Maendeleo, wasikie na waone'
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.