Wakulima wa zao la ufuta mkoa wa Lindi wamefanikiwa kujipatia fedha jumla ya Tsh. 111,838,595,926/= baada ya kufanya mauzo ya jumla ya kilo 49,885,228 za ufuta kwa msimu wa mwaka 2021. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab R. Telack alipokuwa akizungumza na wadau wa mazao ya ufuta na korosho kwenye kikao kilichofanyika jana tarehe 18 Septemba 2021, ukumbi wa ofisi yake.
Akizungumza na wajumbe wa kikao hicho, Mhe. Telack amewapongeza wakulima kwa kuzalisha jumla ya kilo 49,885,228 za ufuta ingawa hayakufikiwa malengo yaliyopangwa ya kuzalisha jumla ya kilo 68,500,000.
Mhe. Telack licha ya kuwapongeza wakulima wa mkoa wa Lindi, amewataka wawe na mpango wa matumizi bora ya fedha walizopata ikiwemo kuweka malengo ya maendeleo, kugharamia elimu za watoto wao, kujenga makazi bora na kuwekeza kwenye shughuli zingine za maendeleo.
Mhe. Telack amevitaka vya vya msingi (AMCOS) vilivyoko Wilaya za Kilwa na Liwale vya Mbwemkuru, Naujombo, Minaki na Nachiungo ambavyo bado vinadaiwa na baadhi ya wakulima, zihakikishe wakulima hao wanalipwa haraka iwezekanavyo.
Kuelekea kwenye msimu wa ununuzi wa korosho, Mhe. Telack amevitaka Vyama Vikuu vya RUNALI na MWAMBAO kuhakikisha kabla ya mnada wa kwanza kutangazwa, vifaa vya kupima unyevu wa korosho viwe vimesambazwa kwa vyama vya msingi ili kudhibiti ukusanyaji wa korosho mbichi. Akitangaza vita na walanguzi, Mhe. Telack amewataka wakulima kuwa wavumilivu na kuacha kuuza korosho zao kwa walanguzi (chomachoma) na badala yake wauze kwenye mfumo rasmi wenye bei nzuri.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.