Leo Wakuu wa Wilaya wateule Mhe. Hassan Ngoma na Judith Nguli wameapishwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab R. Terack katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi. Mhe. Hassan Ngoma rasmi anaanza kazi ya Ukuu wa Wilaya ya Ruangwa na Mhe. Judith Nguri akikabidhiwa majukumu ya Ukuu wa Wilaya ya Liwale. Wah. Wakuu wa wilaya hao wameapishwa leo baada ya kuteuliwa rasmi na Mhe. Rais tarehe 19 Juni 2021 kushika nafasi hizo za kuwaongoza wananchi wa Wilaya za Ruangwa na Liwale.
Aidha, baada ya kuwaapisha Wakuu hao wa Wilaya, Mhe. Zainab R. Terack pamoja na kuwapongeza kwa kuteuliwa na Mhe. Rais amewataka kutumia nafasi hiyo kuwatumikia wananchi vizuri kwa kushirikiana na Makatibu Tawala wa Wilaya na watendaji wengine. Amewaeleza kuwa Ukuu wa Wilaya ni kazi ya kufahamu mambo yote ikiwemo kilimo, mifugo, kilimo cha mwani, afya, miundombinu, elimu nk, hivyo inapaswa kusimamia vizuri miradi ya serikali na maendeleo kwa ujumla .
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Mhe. Makwinye amewaasa Wakuu wa Wilaya kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia ilani ya CCM ikiwemo kufanya kazi kwa ushirikiano na viongozi wa CCM.
Kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Lindi, Mhe. Hassan Ngoma ameahidi kufanya kazi usiku na mchana ili kufikia malengo ya maendeleo kwa kuzingatia miongozo, taratibu, sheria na kanuni za serikali na chama tawala, CCM.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.