Jumla ya wanafunzi 643 wa kidato cha sita katika Mkoa wa Lindi watafanya Mtihani wa Taifa utakaofanyika kuanzia tarehe 02/05/2017 mpaka tarehe 15/05/2015 katika shule 5.
Wanafunzi hao ambao kati yao wasichana ni 540 na wavulana ni 103 Watafanya mtihani huo katika shule za sekondari za Liwale, Lindi, Mbekenyera, Nachingwea na Mahiwa. Tahasusi (combination) zilizopo katika shule hizi ni pamoja na HGL, HKL, HGK, EGM, PGM, PCM, PCB na CBG.
Haya yamesemwa na Kaimu Afisa Elimu Mkoa, Ndg. Friday Sondas huku akiongeza kuwa Mkoa umeshafanya maandalizi yote ya msingi yanayotakiwa. Hivyo amewasihi wanafunzi kujiweka vizuri katika maandalizi yao ya mwisho.
“Ni matumaini yangu kuwa vijana wamefanya maandalizi mazuri na kwamba wapo tayari kwa mitihani”, alisema Sondas. Pia amewasihi wazazi na walezi kuwapa ushirikiano wa kutosha wanafunzi katika kipindi hiki cha mitihani.
Katika Mtihani wa Kidato cha sita wa mwaka 2016 Mkoa wa Lindi ulishika nafasi ya 5 Kitaifa kati ya Mikoa 27 ambapo jumla ya wanafunzi 602 walifanya mtihani na kati yao waliofaulu daraja la kwanza ni 61, daraja la pili ni 301, daraja la tatu ni 213, daraja la tatu ni 21 na daraja la 0 ni 6.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.