Wanalindi wahamasishwa kutumia TTCL
Wananchi wa mkoa wa Lindi wamehamasishwa kutumia mtandao wa TTCL pamoja na huduma zake mbalimbali ili kujiletea maendeleo.
Hamasa hii ilitolewa na mkurugenzi mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Rudi Nyumbani Kumenoga” kwa mkoa wa Lindi iliyofanyika katika uwanja wa Ilulu na kuzinduliwa na Mhe. Godfrey Zambi, Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Kindamba alisema kuwa kuanzia tarehe 01 Julai 2018 TTCL inapatikana nchi nzima kwa teknolojia za 2G, 3G na 4G na inapatikana kwa aina zote za simu. Laini za TTCL ni bure na vocha zinapatikana kwa wingi katika vituo na mawakala nchi nzima.
Pia TTCL inaendelea kufanya maboresho na uwekezaji katika teknolojia na miundombinu kote nchini. Shirika limeazimia kuwa mtandao pekee unao wafikia wananchi wote popote walipo hata katika maeneo ambayo hayaoneshi mvuto wa kibiashara na yale ambayo bado hayajafikiwa na huduma za mawasiliano.
Shirika linatoa huduma ya T Pesa ambayo ilizinduliwa rasmi tarehe 18 Julai 2017. Huduma hii ya kifedha T Pesa imekuwa na mchango mkubwa sana katika kurahisisha huduma za kifedha kwa wananchi, sambamba na kuongeza usalama wa fedha nchini.
Naye Mhe. Zambi aliwaeleza wananchi kuwa TTCL Mpya na kauli mbiu ya “Rudi Nyumbani Kumenoga” ina lengo la kuamsha uzalendo miongoni mwa watanzania ili kuwajulisha kuwa shirika lao lipo makini na imara katika kuwahudumia, likiwa na bidhaa muhimu na huduma bora, salama na nafuu.
Pia amewapongeza TTCL kwa kutambua fursa zilizopo katika mkoa wa Lindi na kuamua kuja kuunga mkoano jitihada zinazoendelea kufanyika na serikali katika kutoa huduma kwa wananchi. Vilevile amewapongeza kwa kuweza kutoa gawio la shilingi bilioni 1.5 kwa serikali ambayo ilikuwa ni sehemu ya faida.
“Niwaombe TTCL kuongeza kasi ya usambazaji wa mawasiliano hasa maeneo ya vijijini kwani katika mkoa wa Lindi bado vipo vijiji vingi ambayo ukienda hupati mawasiliano ya mtandao wowote na wananchi wanauhitaji mkubwa wa mawasilino”, alisema Mhe. Zambi.
Aidha, aliwasihi TTCL kuingia kwenye ushindani kwa kuhakikisha wanatoa huduma iliyobora na kwa bei nafuu ili wanalindi na watanzania kwa ujumla waweze kumudu gharama na kufurahia huduma za kampuni yao.
Mhe. Zambi pia amewasihi wananchi wa mkoa wa Lindi kujiunga na kutumia mtandao wa TTCL ambao kwa sasa umeboreshwa na unatoa huduma bora. Pia amewataka kuchangamkia fursa za ajira kwa kujiajiri wenyewe kuwa mawakala na watoa huduma mbalimbali zitolewazo na TTCL. Faida ya TTCL ni mahususi kwa ajili ya kuboresha huduma za jamii kwa maslai mapana ya wananchi wote na taifa kwa ujumla.
Katika uzinduzi huu, wananchi walipata burudani mbalimbali za muziki wa kizazi kipya kutoka kwa msanii Shilole na Dula Makabila.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.