Wananchi watakiwa kuchukua tahadhari Kimbunga cha Kenneth
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Godfrey W. Zambi leo Alhamisi tarehe 25/4/2019 amesitisha shughuli za umma kwa muda kutokana na tahadhari ya kujikinga na Kimbunga Kenneth kinachotarajiwa kupita katika mikoa ya Lindi na Ruvuma kuanzia tarehe 25-27 Aprili, 2019. Agizo hili la kusitisha shughuli za serikali halitowahusu watumishi wanaohusika na masuala ya uokoaji wakiwemo wa Idara ya Afya, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza na Jeshi la Akiba.
Kutokana na kuwepo kwa matarajio ya kupita kwa kimbunga hiki, Mhe. Zambi ameagiza yafuatayo:-
“Niwaombe wananchi kuzingatia maelekezo yote wanayopewa kuhusu kuchukua tahadhari juu ya uwezekano wa kuwepo kwa kimbunga hiki kwani kwa kutofanya hivyo madhara yanaweza kutokea”, alisema Mhe. Zambi.
Aidha, amewasihi wananchi wote wa mikoa ya Lindi na Ruvuma kuwa watulivu muda wote wakati serikali ikiendelea kufuatilia kwa karibu na kujiandaa kutoa misaada ya kibinadamu endapo maafa yatatokea.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi
Sanduku la Posta: P.o Box 1054 Lindi
Simu: 023-220-2098
Rununu:
Barua pepe: ras.lindi@tamisemi.go.tz
Hati miliki ©2017 Lindi . Haki zote zimehifadhiwa.